HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 11, 2018

BancABC Tanzania yaja na kadi ya YUAN Pre-Paid

Itakuwa benki ya kwanza ya nchini kuwa na kadi ya visa ya YUAN malipo ya kabla.

Wafanyabiashara wanaotembelea Uchina mara kwa mara na wanafunzi kufaidika wanaosafiri kwenda China.

Dar es Salaam, Jumatano 10 Oktoba 2018… BancABC Tanzania ambayo ni kampuni tanzu ya Atlas Mara na ambao imeorodhesha kwenye soko la hisa la London, imepiga hatua nyingine kwenye soko kwa upande wa ubunifu kwa kuja na kadi ya malipo ya kabla – YUAN pre-paid Visa card, ambayo itawawezesha kufanya malipo kwa kwa fedha za China. Kwa sasa BancABC Tanzania inazo kadi 5 za malipo ya kabla ambazo zinapatikana kwa fedha ya USD, Tanzania, Uingereza, Ulaya na Afrika Kusini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutambulisha kadi hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Digitali BancABC Silas Matoi alisema kuwa China imekuwa ni kati ya nchi mashuhuri kwa maswala ya biashara duniani ambapo pia wafanyabiashara wadogo na wakubwa pamoja na wanafunzi kutoka nchini Tanzania wamekuwa wakitembelea kwa wingi ndio maana BancABC ikaamua kuja na kadi ya malipo ya kabla ya YUAN ili kutoa suluhisho hasa pale wanapokuwa wanahitaji fedha ya China.

Kadi ya YUAN ni kadi maalum ambayo inawafanya watumiaji waweze kupata fedha za Uchina kwa thamani ile ile ambayo imewekwa kwenye kadi yake na hivyo itapunguza sana changamoto za kubadilisha fedha ambazo wafanyabiashara na wanafunzi wamekuwa wakikumbana nazo pale wanapohitaji fedha za Uchina wakiwa China au popote pale duniani, alisema Matoi.
 
Matoi aliongeza kuwa ‘Kadi ya YUAN imeundwa kwa umakini mkubwa kwa mfumo salama wa chip na PIN wenye teknolojia ya hali ya juu ambayo inatumika duniani kote na hivyo kuondoa tatizo la kuibiwa. YUAN kadi pia ina huduma ya kupokea ujumbe mfupi wa maneno na hivyo kumfanya mmliki kupata taarifa zote kwa kila muamala au malipo anayofanya kwa kutumia njia ya mtandao.

YUAN kadi haina na makato yeyote ya mwezi na hivyo kuwa na gharama nafuu kwa wateja wetu, alisema Matoi huku akiongeza kuwa mzazi mwenye motto ambaye yuko masomoni China anatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti ya motto wake yenye fedha za Uchina na papo hapo salio litaonekana kwenye kadi ambayo motto anamiliki.

Alisema kuwa BancABC Tanzania ilishinda tuzo ya VISA mwaka 2016 kwa kuongoza kwenye huduma ya malipo ya mtandaoni na mpaka sasa hivi bado inashikilia tuzo hiyo. ‘Tuzo ya VISA tuliweza kushinda kutokana na kuwa na kadi zetu za malipo ya kabla ambazo zimejenga imani kwa wateja wetu pamoja na watumiaji wengine’, aliongeza Matoi.

Hakuna haja ya kuangaika wapi unaweza kutumia kadi ya YUAN kwani inapatikana maasaa 24 kwa siku saba za wiki kwenye ATM za Visa milioni 2.7 duniani kote na kwenye maduka 46 ya reja reja ulimwenguni kote huku kwa Tanzania ikipatikana kwenye ATM za Visa 400 na maduka yayokubali kadi ya Visa 1000.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Wanafanyabiashara Joyce Malai BancABC alisema kuwa kuzindua kadi hiyo ni hatua nyingine kubwa kwa benki hiyo kuendelea kutoa huduma bora na zenye kutoa suluhisho kwa wateja. YUAN kadi bali na kuokoa muda kwa wateja wetu lakini pia inaondoa matumizi ya fedha yasiokuwa ya lazima kwani mteja anaweza kutumia kiasi kile tu ambacho kimehifadhiwa kwenye akaunti yake.

Malai aliongeza kuwa kutokana na huduma bora na nafuu ambazo benki BancABC imekuwa ikizitoa, benki hiyo ilishinda tuzo ya Best Emerging Bank – East Africa kwenye tuzo za The Banker, East Africa Awards 2017. Imekuwa ni moja ya lengo letu sisi kama benki kuendelea kushinda tuzo mbali mbali kuja na huduma zenye ubunifu wa kuwa suluhisho kwa wateja wetu, alisema Malai.
Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya BanABC, Silas Matoi (kulia), na Mkuu wa Wateja Binafsi na wateja wafanyabiashara wa kati na wadogo, Bi. Joyce Malai, wakionyesha mfano wa kadi ya ATM ya fedha za kichina wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa kadi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya BanABC, Silas Matoi (kulia), akizungumza katika hafla ya ya uzinduzi rasmi wa kadi ya ATM ya fedha za kichina ya Visa  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wateja Binafsi na wateja wafanyabiashara wa kati na wadogo, Bi. Joyce Malai.

No comments:

Post a Comment

Pages