Meneja
Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite (kushot0),
akimkabidhi, Rais wa Shirikisho la Mipira wa Kikapu Tanzania (TBF),
Phares Magesa, sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya
Sh. Mil.15 vilivyotolewa na benki hiyo kwa timu za kikapu za Savio na
Lioness zilizo chini ya Kituo cha Vijana cha Don Bosco, Upanga jijini
Dar es Salaam.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite (wa pili kushoto), akimkabidhi, Rais wa Shirikisho la Mipira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa, sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Mil.15.
Rais wa TBF, Phares Magesa, akifurahia zawadi.
Makabidhiano.
Kushukuru.
Kukabidhi vifaa vya michezo.
Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Ali Ngingite (katikati), akimkabidhi, Rais wa Shirikisho la Mipira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa, sehemu ya msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Mil.15 vilivyotolewa na benki hiyo kwa timu za kikapu za Savio na Lioness zilizo chini ya Kituo cha Vijana cha Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NMB tawi la Muhimbili, Happiness Mengi. (Picha na Francis Dande).
NA SALUM
MKANDEMBA
BENKI ya NMB, imewapiga tafu mabingwa wa Ligi ya
Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam, timu za Savio na Lioness zinazomilikiwa na Kituo
cha Vijana cha Don Bosco, kwa kuzipa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Mil. 15.
Msaada huo umekabidhiwa leo Okotba 11, 2018, katika hafla
iliyofanyika Don Bosco, Upanga jijini Dar es Salaam, ambako Rais wa Chama cha
Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Phares Magesa, alipokea msaada huo (mipira,
jezi na mabegi) kwa niaba ya uongozi wa Don Bosco.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja
Mwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Ali Ngingite, alisema wanaamini msaada huo
kwa Savio na Lioness
utakuwa chachu ya mafanikio kwa timu za Don Bosco na
mchezaji mmoja mmoja.
Ngingite alibainisha kuwa, NMB ni washirika wazuri
katika Sekta ya Michezo, ambako wamesaidia, kufadhili na kudhamini timu
mbalimbali ikiwemo Taifa Stars na Azam FC, na sasa wanajisikia fahari kusaidia
kutimiza ndoto za vijana kupitia michezo.
Kwa upande wake, Magesa aliishukuru NMB kwa msaada
huo, lakini akaenda mbali zaidi kwa kuwataka Savio na Lioness kuutumia kama
chachu ya kuendeleza ubora uliowapa ubingwa wa mkoa kwa kupambana kutwaa
ubingwa wa Taifa na Kanda ya Tano Afrika.
“NMB hapa hamjakosea, mmetoa msaada kwa mabingwa wa
mkoa wa Dar es Salaam. Naamini msaada huu utawaongezea morali ya kupigania
ubingwa wa Taifa, michuano ambayo itaanza hivi karibuni na tunawaalika NMB kuja
kudhamini,” alisema Magesa.
Naye Mkurugenzi wa Don Bosco, Padri Michael Muia,
aliipongeza NMB kwa kupokea ombi lao na hatimaye kuwasaidia vifaa hivyo na
kwamba msaada huo umetolewa wakati sahihi, huku akiahidi kuvitunza ili
kuvitumia kwa muda mrefu.
No comments:
Post a Comment