Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, akitoa shukurani zake kwa Kampuni ya SBC iliyodhamini wanariadha wa Tanzania watakaofanya vizuri kwenye mbio za
Rotary Dar Marathon zitakazofanyika Oktoba 14 jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Katibu wa Kamisheni ya Wanariadha, John Jilala na Katibu
Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala.
Meneja Mafunzo na Uwezeshaji wa Kampuni ya SBC, Rashid Chenja, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu udhamini wao kwa wanariadha wa Tanzania watakaofanya vizuri kwenye mbio za Rotary Dar Marathon zitakazofanyika Oktoba 14 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Kamisheni ya Wanariadha, John Jilala na Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo, akitoa ufafanuzi wa njia zitakazotumika katika mbio Rotary Dar Marathon.
NA SALUM
MKANDEMBA
OFA ya kushiriki wa Mashindano ya Beirut Marathon,
zitakazokimbiwa mjini Beirut, nchini Lebanon, Novemba mwaka huu, imetakiwa
kutumiwa kama chachu na wanariadha wa Tanzania kufanya vema katika Rotary Dar
Marathon 2018.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Msaidizi wa
Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Ombeni Zavala, wakati wa kutangazwa rasmi
kwa ofa hiyo iliyotolewa na Mdhamini Mkuu wa Rotary Dar Marathon, Kampuni ya
SBC Tanzania Limited, inayozalisha vinywaji vya Pepsi, Mirinda, 7up na Evervess.
Kwa mujibu wa Mama Zavalla, Watanzania wa kwanza kwa
wanaume na wanawake katika Rotary Dar Marathon, zitakazofanyika Oktoba 14 mwaka
huu, watashinda ofa ya kukimbia Beirut Marathon, kwa gharama za Pepsi.
Alibainisha ya kwamba, hiyo ni ofa muhimu inayopaswa
kuwachagiza wanariadha wa Tanzania kushinda mbio hizo, ili kujitwalia zawadi za
ushindi na kwenda Lebabon, kushiriki Beirut Marathon, zinazoshirikisha
wanariadha maarufu.
“Tunawashukuru Pepsi kwa ofa hii, sisi kama RT
tunatoa wito kwa wanariadha wa Tanzania kuhakikisha wanakimbia na kushinda
Rotary Dar Marathon, ili kupata fursa ya kwenda Lebabon. Tunaamini
hawatotuangusha,” alisema Zavala.
Kwa upande wake, Rashid Chenja, ambaye ni Meneja
Mafunzo na Uwezeshaji wa SBC Tanzania, alisema kampuni yake inajisikia fahari
kubaki mdhamini mkuu kwa miaka 10 sasa na kwamba ofa yao ni sehemu ya
kuadhimisha hilo.
Alisema wameona wawasapoti wanariadha wazawa, ili
kurejesha sehemu ya pato litokanalo na kuungwa mkono kwa bidhaa zao
kunakofanywa na Watanzania, ili kuwachagiza kuibuka na ushindi na kunyanyua
heshima ya Taifa.
“Washindi wa kwanza hadi wa 10 watazawaadiwa pesa,
lakini sisi tukaona tutoe ofa ya safari iliyogharamiwa kila kitu kushiriki
Beirut Marathon na ofa hii itamuhusu Mtanzania wa kwanza kwa wake na waume,”
alisema Chenja.
Alifafanua kwamba, iwapo washindi wa Rotary Dar
Marathon watakuwa sio Watanzania, basi Mtanzania wa kike ama kiume
atakayechomoza nafasi ya juu, hata akiwa nafasi ya tatu, nne, tano ama ndani ya
10 bora, atatwaa ofa hiyo.
No comments:
Post a Comment