*Awe ameshatoa fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu
WAZIRI MKUU Kassim ametoa
siku 10 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Bw. Peter
Swea awe ametoa fedha za mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na
walemavu.
"Leo
ni tarahe 10 nataka hadi ikifika tarehe 20 ya mwezi huu uwe umeshatoa
fedha za mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu. Habari za mpaka kikao
kiridhie hayo ni mambo ya zamani na ndio maana ikatungwa sheria kwa
ajili ya jambo hilo. "
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati
akizungumza na wananchi wa kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mara baada
ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kibakwe, akiwa katika ziara yake
ya kikazi mkoani Dodoma.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mkurugenzi huyo kumueleza kuwa bado
hajatoa fedha kwa ajili ya mikopo hiyo ambazo alipaswa kuzitoa kila robo
mwaka, akidai bado kikao cha kuidhinisha hakijakaa.
Amesema
fedha hizo ambazo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa
kwenye halmashauri, ambapo anatakiwa kutumia asilimia nne kwa ajili ya
mikopo ya wanawake, asilimia mikopo kwa ajili ya vijana na asilimia
mbili zitolewe kwa walemavu.
Kadhalika,Waziri
Mkuu amewaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye
misitu na vyanzo vya maji pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wote
watakaobainika kukata miti bila kibali.
Amesema
mtu yeyote atakayebainika kukata miti bila kibali achukuliwe hatua kali
kwa sababu wamekuwa wakisababisha ukosefu wa maji, ambapo wakandarasi
wa maji kwenye wilaya hiyo wanapata changamoto ya kukosa maji kwenye
maeneo mengo wakati awali Mpwapwa awali ilikuwa na ardhi ya chepechepe.
"Nimepata
habari, hapa Kibakwe watu wanakata miti ili kushindana ubavu wao wa
kuishi. Nawaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yenye vyanzo
vya maji na misitu na muyalinde. Madiwani pia mnatakiwa kushiriki
kukemea ukataji miti.”
Kwa upande wake,
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Jabir Shekimweli ameishukuru Serikali
kwa kutenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo
vitatu vya afya ambavyo ni Kibakwe, Mima na Pwaga.
Amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na kamati za ujenzi kwenye kata na vijiji husika kama ambavyo muongozo ulivyoelekeza.
NayeMbunge
wa Jimbo la Kibakwe, Bw. George Simbachawene amesema utekelezaji wa
Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefanyika kwa mafanikio makubwa
kwenye sekta ya afya, umeme na elimu.
Mbunge
huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, ameomba
ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kongwa, Mpwapwa hadi
Kibakwe, uharakishwe ili kuondoa adha ya miundombinu inayowakabili
wananchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATANO, OKTOBA 10, 2018.
No comments:
Post a Comment