WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amesema atatuma timu maalum kuchunguza wizi
unaofanyika kupitia ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya wilaya ya
Mpwapwa na kwamba hakuna atakayethubutu kuharibu ushahidi kwa kuwa
nyaraka zote za ukusanyaji anazo.
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akizungumza na wafanyakazi
wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Dodoma.
Amesema
hayo baada ya kubaini ubadhirifu kwenye makadirio na ukusanyaji wa
mapato unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Idara ya Fedha na Mipango
kwenye Halmashauri hiyo.
Waziri
Mkuu amesema maeneo ya ubadhirifu ambayo ambayo ameyabaini ni katika
ukusanyaji wa ushuru wa samaki kwenye bwawa la Mtera, Kituo Kikuu cha
Mabasi Mpwapwa na kwenye ushuru wa mabango na majengo.
Amesema
katika halmashauri hiyo kuna genge la wabadhirifu, ambalo ndilo
lililosababisha kufukuzwa kazi kwa Mkurugenzi wa awali wa halmashauri
hiyo, ambapo sasa hawatoi ushirikiano kwa Mkurugenzi aliyekuwepo Bw.
Peter Swea kwa kuwa amedhibiti mianya ya ubadhirifu.
Waziri
Mkuu akiwa kwenye mkutano huo alimtaka Afisa Mipango wa halmashauri
hiyo kusimama na kueleza namna anavyokadiria na kukusanya mapato. "Afisa
Mipango hebu tueleze namna unavyopanga katika kukadiria na kukusanya
mapato, je unakwenda field "eneo la kazi" au unabandika tu makadirio
kwenye makaratasi," amehoji.
Afisa
Mipango huyo alieleza kuwa huwa anakwenda kwenye eneo la tukio kabla ya
kuandaa makadirio ya mapato na baada ya kutoa maelezo hayo Waziri Mkuu
akaeleza namna makadirio na ukusanyaji mapato yaliyofanyika kwenye
ushuru wa samaki.
“Katika
mwaka wa fedha 2016/2017 ilikadiriwa kukusanywa sh. milioni 80 lakini
fedha zilizokusanywa ni sh. milioni 32 na kwenye mwaka wa fedha
uliofuata makadirio uliyashusha kwa asilimia 50 lakini fedha
zilizokusanya ni sh. milioni 109.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu amesema kwenye ushuru wa mabango kwa mwaka wa fedha
2016/2017 walikadiria kukusanya sh. milioni tisa lakini fedha
zilizokusanywa ni sh. milioni moja sawa na asilimia 17. Pia kwenye mwaka
wa fedha 2018/2019 makusanyo yaliyokadiriwa ni sh. milioni saba lakini
hadi sasa hakuna fedha zozote zilizokusanywa.
"Kwenye
ushuru wa majengo mwaka 2017/2018 makadirio yalikuwa kukusanya sh.
milioni 5.5 lakini makusanyo yalikuwa sh.milioni 20 zaidi ya asilimia
360. Hapa tunaweza kusema ulifanya vizuri. Hata hivyo kwenye mwaka huu
wa fedha licha ya makusanyo hayo makadirio yaliyowekwa ni kukusanya sh.
milioni 5.5 lakini hadi jana hakuna fedha iliyokusanywa.”
Waziri
Mkuu amesema kwenye ushuru wa kituo cha mabasi katika mwaka wa fedha
2016/2017 fedha ziliokadiriwa kukusanywa zilikuwa sh. milioni 7.2 na
makusanyo yalikuwa sh. milioni 10.6 sawa na asilimia 148 na katika mwaka
huu wa fedha makadirio yalikuwa sh. milioni 18 lakini hadi jana hakuna
kiasi chochote cha fedha kilichokusanywa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMATANO, OKTOBA 10, 2018.
No comments:
Post a Comment