Mmoja wa wasimamizi wa Ujenzi wa
Jengo la Tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa (JNIA-TB3), Mhandisi
Barton Komba (aliyesimama) akisoma taarifa fupi ya maendeleo ya mradi huo kwa
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Mhe. Elius Kwandikwa leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi
huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa (mwenye shati la
kitenge) akiongea na Wakandarasi na wasimamizi wa mradi wa ujenzi wa jengo la
tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA-TB3), alipokwenda leo kwa ajili ya kukagua maendeleo ujenzi huo.
Mhandisi Barton Komba (kushoto) akimpa maelezo ya mfumo wa mizigo Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius
Kwandikwa (wapili kulia) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi
huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Bw. Richard Mayongela.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Richard Mayongela (kulia) akimuonesha Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa eneo la maegesho ya magari
katika jengo la tatu la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA-TB3), leo alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi huo,
ambao umefikia asilimia 83.
No comments:
Post a Comment