Kamishna Msaidizi na Msemaji wa
Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa akinyanyua juu moja ya bunda la Dola za
Kimarekani zilizokamatwa leo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA), zikisafirisha isivyo halali na raia wa Sudan Kusini Bi. Nada
Zaelnoon Ahamed na Bw. Mohamed Belal, raia wa Syria.
3.
_SAM1125:
4.
_SAM1138:
5.
_SAM1149:
6.
_SAM1175:
Jumla ya Dola za Kimarekani 70,000
sawa na Tsh. milioni 156 za Kitanzania zikiwa zimekamatwa leo kwenye Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), zikisafirishwa na Raia
wawili wa Syria Bw. Mohamed Belal na Bi. Nada Zaelnoo Ahamed raia wa Sudan
Kusini kwa kutofuata taratibu.
Raia wa Syria, Bw. Mohamed Belal
(31) mwenye fulana nyeupe akiwa mbele ya waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA), baada ya kukamatwa na dola 10,000 za Kimarekani, ambazo
hakuzitolea taarifa kwa Maafisa wa Forodha wa kiwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kushoto) akimsikiliza
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa (aliyesimama) alipokuwa akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari leo ya kukamatwa kwa Raia wawili wa Sudan
Kusini na Syria waliokuwa wakisafirikisha fedha taslim milioni 156 bila kufuata
sharia.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela (wa pili kulia)
akisisitiza jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani)
uliofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha
ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakati walipokamatwa Raia wawili
wa Syria na Sudan Kusini wakisafirisha mamilioni ya fedha bila kufuata
taratibu.
Bi.Nada Zaelnoon Ahamed (38) Raia wa
Sudan Kusini (katikati mwenye ushungi) akiwa mbele ya waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kukamatwa na dola 60,000 za
Kimarekani na Paundi 3410 za Sudan.
Na Mwandishi Wetu
ABIRIA wawili Raia wa Sudan Kusini na Syria leo
wamekamatwa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakisafirisha
fedha taslim dola 70,000 za Kimarekani sawa na shilingi milioni 156 za Kitanzania na
paundi 3410 za Sudan bila kufuata taratibu.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa Jengo la Pili la abiria la JNIA, Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Msaidizi, Barnabas Mwakalukwa alimtaja Raia wa Sudan Kusini Bi. Nada
Zaelnoon Ahamed (38) mwenye hati ya kusafiria namba P01563534 amekamatwa saa
10:00 jioni akiwa eneo la ukaguzi wakati akiingia ndani tayari kusafiri kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ 485) akielekea Nairobi.
Hatahivyo, Afande Mwakalukwa amesema abiria huyo mbali na
fedha hizo za Kimarekani pia amekamatwa na paundi za Sudan 3410, ambazo zote
kwa pamoja alishindwa kutoa taarifa ya fedha alizokutwa nazo kwa mujibu wa sheria
ya utakatishaji fedha ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Pia
alimtaja Bw. Mohamed Belal (31), Raia wa Syria mwenye hati ya kusafiria namba
003-16L096876 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya Shirika la ndege la Ethiopia (ET
864) kuelekea Syria kupitia Addis Ababa amekamatwa na dola za kimarekani 10,000
sawa na Tsh. milioni 20 za Kitanzania, ambazo naye alishindwa kuzitolea
taarifa.
“Watuhumiwa
wote wawili wamezuiwa na hawawezi kuendelea na safari zao kwa ajili ya
uchunguzi zaidi na hatua za kisheria zilizopo,” amesema Afande Mwakalukwa.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela amewapongeza maafisa usalama wa JNIA kwa kufanya kazi kwa weledi na
uadilifu pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama katika
kuhakikisha wasafiri, wadau na maeneo yote ya viwanja vya ndege yanabaki salama
na vitendo vya kiuhalifu havina nafasi katika viwanja hivyo.
Bw.
Mayongela amesema pamoja na watumishi hao kufanya kazi katika wakati mgumu
kutokana na baadhi ya abiria kuwa watata kila wanapotaka kutekeleza wajibu wao
kwa mujibu wa sheria na kanuni.
Ametoa
wito kwa wadau, wasafiri na wafanyakazi wote kushirikiana na maafisa usalama,
vyombo vya ulinzi na usalama katika kutoa taarifa stahiki ili vitendo vya
kiuhalifu kama hivi visipate nafasi kwenye viwanja vya ndege kwani ndio vinatoa
taswira ya nchi.
“Viwanja
vya ndege visitumike kama uchochoro wa kupitisha nyara za serikali, dawa za
kulevyia, fedha haramu au matukio yeyote yanayoashiria uvunjifu wa Amani au
uvunjaji wa sheria za nchi,”
Pia
aliongeza “Niombe wananchi na vyombo vya usalama kufanya kazi kwa weledi kwa
sababu wasipofanyakazi kwa weledi matukio kama haya yangeweza kupata nafasi na
kuharibu taswira ya nchi, kwa ujumla mwisho wa siku inaharibika, kwani nia yetu
na lengo letu ni zuri ni kuhakikisha hatutumiki kwa namna moja au nyingine
kufadhili au kuwezesha shughuli za kiuhalifu zifanyike katika maeneo yetu”.
Amesema
na hii ni moja ya ushahidi maafisa usalama wanapata mafunzo na kujengewa uwezo
wa kuwa na vifaa vya kisasa kwani vitu mbalimbali vimekuwa vikigundulika
kupitia mashine za ukaguzi, na pia kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama, hivyo ametoa wito watu wasidhubutu tena kujaribu kwa namna yeyote ile
akidhani viwanja vya ndege wamelala, kwani ulinzi na usalama unaendelea kuimarika.
Kwa
upande wake Meneja wa Forodha wa Kituo cha JNIA, Bw. Njaule Mdendu amesema
abiria wote wanaosafiri au kuwasili endapo wanakiasi kikubwa cha fedha za
kigeni kuanzia dola 10,000 za Kimarekani sawa na Milioni 10 za Kitanzania
anapaswa kutoa taarifa Idara ya Forodha kwa kuwa ni matakwa ya sheria ya mwaka
2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012 na kanuni za mwaka 2016, na asipofanya
hivyo ni kosa la jinai.
Bw.
Mdendu amesema abiria wanapaswa kuchukua fomu maalum akieleza utambulisho wake
na kiasi cha fedha anachoingia nacho au kutoka nacho, na fomu atazipata kwenye
ofisi zote za forodha za mipakani kwenye viwanja vya ndege, mipaka ya ardhi na
majini endapo atakuwa akitumia usafiri wa barabara au majini.
“Hizi
fomu pia zipo kwenye tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania na akishajaza
anawasilisha ofisi za Forodha na kiasi cha fedha anachosafiri au kuwasili nacho
na afisa atazihakiki na akiridhika ataruhusu aendelee na safari yake, na
napenda kuwatoa hofu watu kuwa fedha zao hawanyang’anyi baada ya kutoa taarifa
na ataondoka nayo, lakini endapo usipotoa taarifa ni kosa na inaadhabu yake
kulingana na kiasi cha fedha ulichokutwa nacho, hivyo tuwaombe abiria kutimiza matakwa
ya kisheria, kwani watu wamekuwa wakifanya makosa bila kujua sheria,” amesema.
No comments:
Post a Comment