Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao walifika Ikulu jijini
Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Miguu la Tanzania TFF, BMT
pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars ambao walifika Ikulu jijini
Dar es Salaam pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Miguu la Tanzania TFF, BMT
pamoja na Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya
pamoja na Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Taifa Stars mara baada ya
kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha mstari wa Mbele
ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe watatu
kutoka kushoto, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Dkt. Augustine Mahiga watatu
kutoka kulia akifatiwa na Leodgar Tenga Mwenyekiti wa BMT, kocha wa timu ya
Taifa Emanuel Amunike Pamoja na Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao. Wengine ni
Rais wa TFF Wallace Karia akiwa pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto
Nyoni.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na
Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni mara baada ya kupiga picha ya pamoja na
Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kipa
wa Timu ya Taifa Aishi Manula mara baada ya kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Beki
kisiki wa Taifa ya Tanzania Kelvin Yondani mara baada ya kupiga picha ya pamoja
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Beki wa
Timu ya Taifa Shomari Kapombe akijitambulisha mara baada ya kuwasili Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya
Jezi ya Timu ya Taifa kutoka kwa Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Nahodha wa Timu hiyo Erasto Nyoni mara baada ya
kumkabidhi Jezi ya Timu ya Taifa.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi Shilingi
milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe
pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya
kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace
Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa
Erasto Nyoni.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo mara
baada ya kukabidhi Shilingi milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Maandalizi ya Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment