Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na wa Kati wa Benki ya
Exim, Agnes Kaganda (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo
pichani) kuhusiana na kampeni mpya ya benki hiyo inayofahamika kama ‘Deposit Utokelezee na
Exim’ leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni muendelezo wa benki
hiyo kuwahamasisha watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi. Wengine
ni pamoja na Mkuu wa Kitengo cha wateja wakubwa (corporate) wa benki hiyo, Shrikant Ganduri (kushoto) na Mkuu wa Hazina na Masoko ya Fedha wa benki hiyo
Bw Arafat Haji
Dar es Salaam, Tanzania
Benki ya Exim Tanzania leo imezindua rasmi kampeni yake inayofahamika kama
‘Deposit Utokelezee na Exim’ ikiwa ni muendelezo wa benki hiyo kuwahamasisha
watanzania kujenga tabia ya kujiwekea akiba zaidi.
Kampeni hiyo
iliyozinduliwa jijini Dar es Salaam leo inawawezesha wateja wa benki hiyo
kupata viwango vya riba vya kuvutia hadi asilimia 10.5 ikiwa watafungua akaunti
ya amana maalum (fixed deposit) au kuweka kwenye akaunti zao za amana maalum kiasi
kisichopungua Sh 50m/- kabla ya Desemba 31 mwaka huu..
"Kampeni hii
inalenga kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa watanzania. Kwa kuzingatia
viwango vya ushindani tunavyowasilisha kupitia kampeni hii, wateja wetu watakuwa
na uwezo wa kunufaika na riba ya hadi 10.5% kwenye amana zao, " Alisema
Kaimu Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na wa kati wa Benki ya Exim Bi Agnes
Kaganda wakati hafla fupi ya uzinduzi wa kampeni hiyo iliyofanyika leo jijini
Dar es Salaam.
Kampeni hii inakuja
ikiwa ni mwendelezo wa mkakati wa benki hiyo katika kusimamia ustawi wa wateja unaofahamika
kama 'Exim kazini leo, kwa ajili ya kesho' (Exim at Work Today, for tomorrow) unaoendana
na dira na muelekeo wa benki hiyo. Ni kampeni inayothibitisha nia ya benki ya
Exim katika kutafuta kesho iliyo bora kwa wateja na jamii inayoizunguka.
Bi Kaganda aliongeza,
"kama benki, tunaahidi kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya wateja wetu, ili
kuhakikisha wanakua na ustawi mzuri sasa na hata baadae. Kupitia akaunti zetu za
muda maalum (Fixed deposit) mteja anaweza kuongeza kiasi kikubwa cha pesa huku
akiwa na uhuru wa kuchagua aina ya muda anaotaka. Tunaamini kwamba kesho yako
bora inaanza leo.’’
Tangu
kuanzishwa kwake mwaka 1997, Benki ya Exim imefanikiwa kujitanua maeneo
mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo kwasasa ina matawi yake kwenye mikoa 13
nchini ikiwa ni pamoja na mikoa ya Dar es Salaam, Zanzibar, Tanga, Morogoro,
Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Iringa, Mbeya na
Mtwara. Pia matawi yake yapo kwenye nchi za Comoros, Djibouti na Uganda.
No comments:
Post a Comment