Dk. Mzuri Issa Ali akizungumza na waandishi wa habari katika kikao
maalumu cha kupinga udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto Zanzibar.
Na Talib Ussi, Zanzibar
WANAHARAKATI wa kutetea haki za wanawake nchini wametoa
wito kwa vyombo vya sheria kuharakisha
uchunguzi na kuwaomba pia wananchi kutoa ushirikiano ili kukamilisha kesi za
mauwaji ya wanawake na watoto kwa wakati muafaka
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi
wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa upande
wa Zanzibar, Dk Mzuri Issa Ali katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari wakati dunia vya ukatili wa kijinsia.inaadhimisha
siku 16 za kupinga vitendo
Alieeleza
kuwa kama kesi hizo zikishughulikiwa kwa haraka na taarifa zake kusambazwa
nchini kote itapunguza tabia ya baadhi ya watu ya kuendelea na tabia hiyo kumaliza
maisha ya wanawake na watoto nchi.
Alisema
kwa mwaka huu pekee, tayari wanawake watano na watoto wawili wameripotiwa
kuuawa katika mkoa wa Kusini Unguja lakini bado kesi hizo hazijapatiwa wowote
hadi leo.
Alieleza
kwamba Mei 14, 2018 mtoto Elizabeth Ndaula mwenye
umri wa miaka 8 alikutwa amefariki katika kichaka huko Bambi wilaya ya Kati
Mkoa wa Kusini Unguja pia Mei 22, 2018 Patima Abdallah Makame (27) na mtoto
wake wa miezi mitano Haji Ismail walikutwa wameuawa nyumbani kwao Guruweni Jendele
wilaya ya Kati.
Julai
18 na 31, 2018 msichana Wasila Mussa (21) wahuko Tunguu Kichangani Wilaya ya
Kati pia mwizi huo huo na Agatha Francis Pius mkaazi wa Kiboje Ndagaa wilayani
humo aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali shingoni kwake wakati akienda shamba
saa nne asubuhi.
Novemba 2. 2018 majira ya saa 7:00 usiku Issa Masuli Juma (40)
na mkewe Asha Khamis (20) wote wakaazi wa Kibele wilaya ya kati waliuliwa na watu
wasiojulikana kwa kupigwa na kitu kigumu sehemu ya kichwani nyumbani kwao.
Dk.
Mzuri alieleza kuwa kila wakiwasiliana na jeshi la Polisi wanajibiwa kuwa
uchunguzi uendelea na bado haujakamilika na ukamilika watafikishwa mahakamani.
Pia
inatoa wito kwa jamii kuacha kabisa vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake
kwani vinakwenda kinyume na maadili pia na mipango ya nchi ya kimaendeleo.
Hata
hivyo kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan alisema ushahidi
unashindwa kupatikana na kutokana na jamii kushindwa kutoa ushirikiano.
“Kwa
mfano tukio la mawauji ya Agatha lilitokea mchana kweupe akiwa kondeni, hivi
kweli hakuna mtu aliyona mpaka watu kujitokeza kutoa ushahidiii, kwa kweli
tunakosa ushirikiano” alieleza Kamanda huyo
Maadhimisho
hayo huadhimishwa kila mwaka kuazia Novemba 25 hadi Desemba 10.
No comments:
Post a Comment