Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akitangaza punguzo la bei za tiketi zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kushoto ni Msanii wa Bongo Flava, Mimi Mars na Joh Makini.
Katibu Kiongozi wa msimu wa Tigo
Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote, Gardner Habash (kati) akiwa pamoja na Mkuu wa
Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga na msanii wa Bongo Flava, Fareed
Kubanda – Fid Q (kulia) walipotangaza kuwa wateja wote watakaotumia usafiri wa
Uber Jumamosi hii kwenda kushuhudia kilele
cha tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama lote katika viwanja vya Leaders Club jijini
Dar es Salaam watapokea punguzo la TSH 5,000 kwa usafiri huo.
Msanii wa Bongo Flava Whozu (wa
tatu kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadalizi ya kilele cha tamasha
la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote litakalofanyika Jumamosi hii katika
viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Huduma za Masoko wa
Tigo, William Mpinga (kushoto) alitangaza ofa kabambe kutoka Tigo ikiwemo
punguzo kubwa la bei kwa tiketi zote
zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Msanii wa Bongo Flava, Fareed
Kubanda – Fid Q akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi yake kuelekea
kilele cha tamasha kubwa la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote litakalofanyika Jumamosi
hii katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam . Tigo imetangaza punguzo kubwa la bei kwa
tiketi zote zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
Mkuu wa Huduma za Masoko wa Tigo,
William Mpinga pamoja na Katibu Kiongozi wa msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama
Lote, Gardner Habash (kati) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii
watakaotumbuiza katika kilele cha msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote siku
ya Jumamosi katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Msanii wa Bongo Flava, Mimi Mars
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandilizi ya kilele cha tamasha la
Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote litakalofanyika Jumamosi hii katika viwanja
vya Leaders Club jijini Dar es Salaam. Tigo imetangaza punguzo kubwa la bei kwa
tiketi zote zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR.
NA MAKUBURI
ALLY
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Tigo, imetoa wito kwa mashabiki
wa muziki hapa nchini kujitokeza kwa wingi kwenye Tamasha la Tigo Fiesta Vibe
kama Lote litakalofanyika kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam,
kesho.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana,
Meneja Huduma za Masoko wa Tigo, William Mpinga, alisema onyesho la kesho
litakuwa ni la aina yake zaidi ya matamasha yaliyofanyika katika mikoa 14.
Mpinga, alisema shoo hiyo itakuwa ni ya aina yake zaidi ya
tamasha la mwaka jana, ambako wameamua
kuliboresha zaidi katika ununuzi wa tiketi kwa njia ya Tigopesa Master pass QR.
Aliweka bayana kiingilio ni Sh. 15, 000 watakaolipia getini
siku ya tamasha huku kwa watakaolipa kwa njia ya Tigopesa watalipa Sh. 10,000
na mteja kuingizwa kwenye droo ya Jigiftishe ya Sh. Milioni moja moja kwa siku
na milioni 100 kwa wiki.
Mratibu wa Fiesta, Gadner G. Habash, alisema maandalizi yako
sawasawa, kesho wakazi wa Dar es Salaam na mikoa ya karibu wajitokeze kwa wingi
kushuhudia burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mahiri.
Habash, alisema wasanii wazawa zaidi 30 wanatarajiwa kupanda
katika jukwaa la Fiesta, ikiwa ni orodha ya awali ya tamasha hilo na kwamba,
idadi kamili ya wasanii watakaotumbuiza itawekwa wazi kesho asubuhi na waratibu
wa tamasha hilo.
Kwa upande wa Msanii Whozu, alisema kuelekeza tamasha la
kesho, wamejipanga vilivyo kuwapa burudani ya aina yake, kwani wamejitahidi
kuandaa vitu vipya.
Naye Joh Makini ‘Mwamba wa Kaskazini’, aliwaita mashabiki wa
muziki kujitokeza katika viwanja vya Leaders, kupata burudani ya aina yake
katika tamasha hilo.
No comments:
Post a Comment