HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 27, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI MAKTABA MPYA YA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja. Wengine katika picha wanaoshuhudia ni Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Mama Kate Kamba, Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea mfano wa funguo kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kuashiria ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja huku viongozi wengine wakipiga makofi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya kitabu kilichomo katika Maktaba hiyo mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla hajaifungua rasmi huku Balozi wa China hapa nchini Wang Ke akitazama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya kompyuta zinazohifadhi vitabu (onlinebooks) ambazo wanafunzi watakuwa wakijisomea pamoja na kupata huduma ya mtandao internet.
Taaswira ya moja ya Mashelfu yenye vitabu katika maktaba hiyo mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata maelezo mbalimbali ya  maktaba hiyo mpya itakavyokuwa ikihudimia wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu watakapoanza kuitumia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu Msataafu Edward Lowassa mara baada ya kuwasili katika eneo la Maktaba mpya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baadhi ya Mabalozi  wanaoziwakilisha nchi zao wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla ya kuifungua rasmi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisoma moja ya kitabu cha Sayansi katika maktaba hiyo mpya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Vitabu kutoka kwa Balozi wa China hapa nchini Wang Ke kabla ya ufunguzi wa Maktaba hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla hiyo ya ufunguzi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa mara baada ya kufungua Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 2100 kwa wakati mmoja. Makataba hiyo pia ina Ukumbi mkubwa wa Mikutano wenye viti 600 na uwezo wa kuhifadhi vitabu 800,000.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakicheza pamoja na kwaya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Maktaba hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke wakati wakiagana mara baada ya hafla ya ufunguzi wa Maktaba hiyo ya Kisasa.

No comments:

Post a Comment

Pages