Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Baadhi ya watoto waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani.
Baadhi ya watoto waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani.
NA MWANDISHI WETU
KATI ya watoto 10 wa kike nchini, watatu hufanyiwa vitendo vya ukatili wa kingono huku kati ya watoto saba wa kiume, mmoja hufanyiwa ukatili wa aina hiyo.
Takwimu hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana na a Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya Siku ya Watoto Duniani iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF).
Alisema watoto hao hukumbana na ukatili wa aina hiyo shuleni, nyumbani na kwamba wanafanyiwa vitendo hivyo na watu wao wa karibu.
“Shuleni si salama, nyumbani pia si salama na vitendo hivi hufanyiwa na watu wa karibu, lazima tuseme ukweli. Kila siku napokea simu na meseji nyingi ya watoto kufanyiwa ukatili wa kingono.
“Nawaomba viongozi wa dini tushirikiane kukemea tatizo hili, kwani imeonekana sheria si mwarobaini, pia tutumie hamasa,” alisema.
Pia aliihimiza jamii wanapoona ama kusikia matukio ya ukatili kwa watoto kupiga simu namba 116, kutoa taarifa, ili mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki.
Pamoja na hayo, awalitaka wazazi na walezi kutumiza wajibu wao wa kulea watoto na pia kuwapa fursa ya kuwasiliza katika masuala mbalimbali.
No comments:
Post a Comment