NA TIGANYA VINCENT
UONGOZI wa Kijiji cha Chamalendi katika Kata ya Choma wilayani Igunga umeagizwa kuandaa mkataba wa matumizi ya mashamba yaliyokuwa chini ya Mfuko wa Maendeleo ya Kijiji(MFUMAKI) kwa ajili ya wananchi wanaohitaji kulima msimu ujao ili kuepusha kuendelea kwa migogoro katika eneo hilo.
Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri baada ya kufanikiwa kusuluhisha mgogoro wa kugombea eneo hilo kati ya watu waliokuwa wamekodishiwa eneo hilo kudai ni lao na Uongozi wa Kijiji hicho ambao ndio wamiliki halali.
Alisema kuendelea kuwaachia wananchi kulima katika eneo hilo la Kijiji hicho bila ya kuandaa mkataba utakaoeleza masharti ya kulitumia kutasababisha kuendelea kuwepo kwa migogoro kwa wananchi wanaolitumia kwa muda mrefu kwa kudai kuwa ni lao.
“Ni lazima muweke mkataba na mwananchi anayekodisha sehemu ya eneo hilo utakaonyesha kuwa anakaa kwa muda gani…na pindi mnatakapotaka kuliendeleza anaondokaje…lazima mambo yawe wazi …na eneo hilo wakati bado mnaandaa mipango ya kuliendeleza kwa maslahi mapana ya Kijiji wananchi wanaweza kuendelea kulitumia kwa makubaliano ya Kijiji”alisema.
Alisema kimsingi yeye hana Mamlaka ya kubadilisha matumizi ya eneo hilo na kuongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio mwenye uwezo wa kufanya hivyo na kusisitiza kuwa eneo hilo litabaki kuwa mali ya Kijiji na sio vinginevyo kwa mujibu wa Sheria inavyosema.
Awali Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Chamalendi Adophina Kwimba alisema baadhi ya watu waliokodishiwa mashamba hayo walianza kuyauza na ndipo uongozi wa Kijiji uliamua kuwazuia kueendelea kulima katika eneo hilo na ndipo mgogoro uliobuka kwa baadhi yao kudai ni mali yao.
Alisema Serikali ya Kijiji hicho ililiacha eneo wazi kwa ajili ya kujenga huduma za jamii kama vile shule, kituo cha Afya , soko na Stendi
Kaimu Mkuu wa Idara ya ardhi na Maliasi Afisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Jahulula Edward alisema kuwa eneo hilo ni mali ya Kijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 ambayo ilirudisha mashamba ya MFUMAKI na yale ya Bega kwa Bega katika usimamizi wa Kijiji husika.

No comments:
Post a Comment