HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 29, 2018

WATEJA WA TIGO SASA WANAWEZA KUFANYA MALIPO KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELETRONIKI WA MALIPO SERIKALINI (GePG)

Ofisa Mwandamizi wa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bernard Mabagala, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Malipo Serikalini kwa njia ya Tigo Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya na katikati ni Mkuu wa Hudumza za Kifedha kwa njia ya Mtandao Tigo, Hussein Sayed.
Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa njia ya Mtandao wa Kampuni ya Tigo, Hussein Sayed, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Malipo Serikalini kwa njia ya Tigo Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Tehama kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bernard Mabagala na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya. 
Mkuu wa Huduma za Kifedha kwa njia ya Mtandao wa Kampuni ya Tigo, Hussein Sayed, akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Kieletroniki wa Malipo Serikalini kwa njia ya Tigo Pesa uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya.

Wateja wa Kampuni ya Tigo, sasa wanaweza kufanya malipo kutumia mfumo wa Kielektroniki wa Malipo Serikalini (GePG) baada ya kampuni hiyo kuongeza malipo ya Serikalini kwenye App yake ya Tigo Pesa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa GePG kwa mtandao wa Tigo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Mwandamizi wa TEHAMA - Wizara ya Fedha na Mipango, Bernard Mabagala,  alisema kuwa ubunifu na juhudi za Serikali katika  kuanzisha mdumo huo wa Kieletronbiki wa Malipo Serikalini (GePG) umerahisisha upatikanaji wa ankara na kufanya malipo kwa wananchi. 

Pia imeleta faida nyinginezo ikiwemo kuboresha uwekaji wa kumbukumbu, utoaji wa taarifa, kupunguza uvuvaji na ubadhirifu pamoja na kuongeza mapato kwa idara mbalimbali za Serikali. 

Kupitia mfumo wa GePG Serikali pia imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma kwa wananchi na kuongeza fursa za biashara kwa kampuni zinazotoa huduma za malipo kama Tigo. Wananchi wanaweza kupokea ankara zao moja kwa moja kutoka ofisi na mashirika ya Serikali au kwa njia mbali mbali za kimtandao, na kufanya malipo ya ankara kwa urahisi na mahali popote kwa njia ya simu za kiganjani, benki au kwa njia ya mtandao. 

“Kufanya kazi kwa karibu na Serikali ili kufikisha huduma za kifedha kwa wananchi wengi ni moja kati ya malengo na mkakati wetu,” alisema Hussein Sayed, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za kifedha wa Tigo.

“Zaidi ya wateja milioni 7 wanaotumia huduma yetu ya Tigo Pesa sasa wana uwezo zaidi wa kufanya malipo kwa haraka kwenda kwa taasisi, Wizara na wakala wa Serikali zaidi ya 300 kupitia Tigo Pesa USSD, Tigo Pesa App na QR Code,” alisema Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Serikali wa Tigo, Ally Maswanya.

Baadhi ya taasisi za Serikali ambazo malipo yanaweza kufanywa kwa Tigo Pesa ni pamoja na Wizara ya Ardhi, Shirika la Kodi Tanzania (TRA), Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, Mamlaka za Miji, Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA), Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Misitu (TFS), Wizara Malia Asili na Utalii, Bodi ya Utalii, Idara ya Uhamiaji, Mamlaka za Maji katika miji ya Mwanza (MWAUWASA), Tanga (Tanga UWASA), Dar es Salaam (DAWASA), Dodoma (DUWASA), Hospitali mbali mbali kama vile Muhimbili, Mwananyamala na idara nyingine zaidi ya 300.

Ili kufanya malipo kwa kutumia Tigo Pesa App na QR Code, wateja wa Tigo wanahitaji kupakua App ya Tigo Pesa na kuscan QR code kisha kuingiza namba ya siri ili kufanikisha muamala.

No comments:

Post a Comment

Pages