Naibu Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt.
Mary Mwanjelwa (Mb) akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kikao cha menejimenti ya
ofisi yake (hawapo pichani) alipokutana nao kwa lengo kufahamiana na kupanga
mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa
huduma bora kwa umma.
Baadhi ya wajumbe
wa kikao cha menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) alipokutana nao kwa lengo
kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi utakaoziwezesha
taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa
(Mb) amewataka watumishi wa ofisi yake kuwa mfano wa kuigwa na taasisi nyingine
kiutendaji kwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa, uadilifu na weledi ili kujenga
misingi bora ya utumishi wa umma nchini.
Mhe. Dkt.
Mwanjelwa ametoa maelekezo hayo leo wakati akizungumza na menejimenti ya ofisi
yake, lengo likiwa ni kufahamiana na kupanga mkakati madhubuti wa utendaji kazi
utakaoziwezesha taasisi za umma nchini kutoa huduma bora kwa umma.
Mhe. Dkt.
Mwanjelwa amesema, watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora, wamepewa dhamana ya kuhakikisha utumishi wa umma unakuwa na
tija na maslahi kwa maendeleo ya taifa hivyo hawana budi kutekeleza wajibu wao
kikamilifu.
Mhe. Dkt.
Mwanjelwa ameongeza kuwa, watumishi wakifanya kazi kwa kuzingatia sheria,
kanuni, taratibu na miongozo ya utumishi wa umma iliyopo, malalamiko yasiyo ya
lazima kwenye eneo la utumishi na utawala bora yatapungua kwa kiwango kikubwa.
Aidha, Mhe.
Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, mtumishi wa umma anatakiwa kupimwa kwa
utendaji kazi wake kwa matokea chanya ili atakapopanda daraja ajivunie utendaji
kazi wake na kuongeza kuwa, upimaji huo utapunguza malalamiko ya kutopandishwa
madaraja kwa watumishi ambao hawawajibiki ipasavyo.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amekutana na menejimenti ya ofisi yake kwa mara ya
kwanza mara baada ya kuripoti na kuanza kazi rasmi tarehe 14 Novemba, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Mhe.
Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 10 Novemba, 2018
na kumuapisha tarehe 12 Novemba, 2018.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE 07 DESEMBA
No comments:
Post a Comment