Wateja wa DStv wanauanza mwaka kwa kicheko baada ya kutangazwa rasmi kuwa DStv itaonyesha michuano maaruya ya Emirates FA Cup kupitia chaneli za SuperSport kuanzia tarehe 4 Januari 2019. Hii inamaana kuwa mechi za mzunguko wa tatu sasa zitaonekana katika kisimbuzi cha DStv
Akizungumzia kurejea kwa michuano hiyo katika chaneli za SuperSport, Mkurugenzi wa MutliChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema “Lengo letu ni kuwa mstari wa mbele katika kutoa burudani ya soka bora duniani kwa wateja wetu wa DStv hivyo, kuanzia tarehe 4 Januari 2019, wateja wetu wataweza kufurahia michuano ya Kombe la Emirates maarufu kama FA Cup kupitia chaneli za SuperSport zizopatikana ndani ya vifurushi vya DStv"
Amesema kuwa muda wote MultiChoice imahakikisha kuwa wateja wake wanapata burudani ya hali ya juu na ndiyo sababu wamekuwa wakiongeza maudhui mapya kila uchao katika vifurushi vya DStv.
Sambamba na mechi za michuano ya kombe la FA za mzunguko wa tatu zitakazoanza Januari 4 2019, wateja wa DStv pia wataendelea kuburudika na ligi kubwa za soka zinazotamba duniani ikiwemo ligi kuu ya Uingereza maarafu kama PL, ligi kuu ya Italia Seria A, michuano ya ligi kuu ya Hispania {La Liga} na ligi ya mabingwa Ulaya maarufu kama EUFA Champions League bila kusahau maudhui mengineyo mengi zikiwamo filamu na tamthilia mpya kutoka nje na ndani ya Tanzania na vipindi vya watoto.
Mechi hizi za michuano ya kombe la FA zitakuwa zikipatikana mubashara kupitia chaneli za Supersport ndani ya DStv. Idadi ya mechi zitakazoonekana mubashara zinatofautian kulingana na aina ya kifurushi huku baadhi ya mechi hizo zikionekana katika kifurushi cha chini cha DStv Bomba kwa Sh 19,000.
Kwa wateja wanaotaka kujiunga na DStv, bado wanaweza kunufaika na ofa inayoendelea ya msimu wa sikukuu ambapo kwa gharama ya Sh.79,000 tu! Mteja anapata seti kamili ya DStv. Pia kupitiamtandao wa bongoshop.dstv.com mteja anaweza kupata maelekezo ya ziada ya namna ya kujiunga na DStv ikiwemo kuunganishwa na mawakala na mafundi wa DStv popote alipo.
No comments:
Post a Comment