Mkurugenzi wa NMB Bank, Ineke Bussemaker, akisalimiana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Dk. Bernard Kibese kwenye hafla fupi ya kumuaga mkurugenzi wa NMB Bank anayemaliza muda wake baada ya kuitumikia benbki hiyo kwa miaka mine.
NA SALUM MKANDEMBA
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker, amehitimisha miaka minne ya utumishi uliotukuka katika benki hiyo na kuagwa mwishoni mwa wiki, huku akifichua kuwa alifanya kazi chini ya vipaumbele kadhaa, kikubwa kikiwa ni kuwawezesha wanawake kukua kiuchumi.
Hafla ya kumuaga Ineke, ilifanyika jijijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wanahisa wa NMB, Wakurugenzi Watendaji na Maofisa Watendaji Wakuu wa taasisi za fedha nchini ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao alishirikiana nao kwa pamoja tangu kuajiriwa kwake.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ineke alisema anamshukuru kila mmoja kwa ushirikiano aliompa kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, na kwamba anaondoka akiwa na furaha kutokana na uimara alioijengea NMB – ambayo inasimama kama benki kinara Tanzania.
Ineke alisema haikuwa rahisi kwake kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake, lakini kutokana na ushrikiano na wadau, wafanyakazi, wakuu wa idara na vitengo, sanjari na mameneja na wakurugenzi, ameiwezesha NMB sasa kufikisha matawi 228, ATM 800 na mawakala 6,000.
“Naomba wadau kuendelea kufanya biashara na sisi ili kutupa nguvu ya kukabiliana na ushindani kuelekea Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati, mchakato ulio chini ya Serikali ya Awamu ya Tano. Lakini pia kujitoa katika kuwawezesha wanawake kiuchumi ili kujenga jamii imara,” added Ms Bussemaker.
Mkurugenzi huyo aliwashukuru viongozi na wafanyakazi wa NMB kwa aina ya ushirikiano waliompa kwa kipindi cha miaka minne ya utumishi na kuhakikisha wanaigeuza benki hiyo kuwa imara kimapato na kiukuaji na kuwa kinara wa taasisi za fedha nchini Tanzania.
“Wakati wa utendaji wangu hapa, nilijaribu kadri nilivyoweza kuhakikisha nawawezesha wanawake kiuchumi na kukua kimapato kuanzia ngazi ya chini hadi juu, lakini pia kuwapa nafasi katika idara na vitengo tofauti ndani ya benki. Natamani kuona hili likiendelea,” alisema Ineke.
Ineke ameiacha NMB katika niia sahihi ya ukuaji kiuchumi na kimapato, ikiwa ndio benki kinara, iliyo na wateja zaidi ya milioni 3 Tanzania, wanaohudumiwa kupitia matawi 228, Mawakala 600 na ATM 800. Wanahisa wakubwa wa NMB ni Rabobank (hisa 34.9%) na Serikali ya Tanzania (31.9%).
No comments:
Post a Comment