Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na watumishi wa Wilaya
ya Mkalama, mkoani Singida leo baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua
shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula, akiwa ndani
ya gari la polisi muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo
pichani), alipokuwa ziara katika Wilaya hiyo, lengo ikiwa ni kukagua shughuli
mbalimbali zinazofanywa na Idara za wizara, mkoani Singida.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na
Askari Polisi wa Kituo cha Nduguti kilichopo Wilayani ya Mkalama, mkoani Singida leo baada
ya kuwasili kwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Allan Kiula(kushoto),
akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kushuhudia gari la
polisi (pichani), lililoletwa kwa ajili ya shughuli za kudhibiti uhalifu, Naibu Waziri yupo mkoani Singida lengo ikiwa ni kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na Idara
za wizara.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akisikiliza maelezo kutoka
kwa Mkuu wa Polisi wilayani Mkalama, John Ntalima, mkoani Singida Leo, ikiwa ziara ya kikazi ya kukagua shughuli
zinazofanywa na Idara zilizopo chini ya wizara.
No comments:
Post a Comment