Mwenyekiti wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (R), SemistoclesKaijage akitoa taarifa kwa umma
kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Ubunge jimbo la Temeke na Udiwani katika kata 46 za
Tanzania Bara.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo
katika Jimbo la Temeke, Mkoani Dar es Salaam na kwenye Kata 46 za Tanzania
Bara.
Akitangaza kufanyika kwa uchaguzi
huo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage
amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika Januari 19 mwaka 2019 na fomu za uteuzi wa
wagombea zitatolewa kuanzia tarehe 14 hadi tarehe 20 Desemba 2018.
"Uteuzi wa Wagombea utafanyika
tarehe 20 Desemba, mwaka huu. Kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 21
Desemba, hadi tarehe 18 Januari, mwaka 2019 na siku ya uchaguzi itakuwa ni tarehe
19 Januari mwaka 2019,” amesema Jaji Kaijage.
Jaji Kaijage amebainisha kuwa Tume
imetangaza uwepo wa nafasi wazi ya Ubunge kwenye Jimbo la Temeke baada ya kupokea
taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai juu ya uwepo wa nafasi wazi ya
Ubunge katika jimbo hilo.
Amesema kuwa Tume ilipokea barua kutoka
kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia kifungu
cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, aliitarifu Tume uwepo wa
nafasi wazi ya Mbunge wa Jimbo la Temeke katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke
Mkoani Dar es Salaam kufuatia Kujiuzulu uanachama wa Chama Wananchi CUF kwa aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Maulid Said
Abdllha Mtolea.
Kwa upande wa nafasi wazi za Udiwani
Jaji Kaijage amesema kuwa Tume ilipokea taarifa
kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali ya Mtaa akiitaarifu Tume juu ya uwepo wa nafasi wazi za Udiwani
katika Kata 46.
“Tume imepokea Taarifa kutoka kwa
Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaaa mbaye kwa kutumia mamlaka aliyopewa
chini ya Kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya
292, aliitarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 46 za
Tanzania Bara,” amesisitiza Jaji Kaijage.
Ametoa wito kwa vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia Sheria, Kanuni,
Maadili ya Uchaguzi, Taratibu, Miongozo na maelekezo yote yatakayotolewa na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakati wa kipindi cha Uchaguzi mdogo.
Jaji Kaijage amefafanua kuwa kuwa uchaguzi
huo mdogo utafanyika ndani ya Halmashauri 28 zilizopo kwenye Mikoa 14 ya
Tanzania Bara.
Halamashauri na Kata zitakazokuwa
na Uchaguzi ni pamoja na Ngorongoro (Sale,Misigyo,Malambo,
Orgosorok na Olorien/Magaiduru), Arusha(Kimnyak),
Kilwa (Kiranje ranje, Kikole, Pande
Mikoana), Liwale (Kata Kichonda na
Mlembwe), Babati(Dareda na Magara, Kiteto(Makame), Simanjiro(Loiborsiret, Ruvu Remit, Naberera), Kwimba(Walla), Sengerema(Nyampulukano),
Ulanga(Msogezi), Mvomero(Mtibwa, Tchenzema, Mangae), Kilosa(Magomeni), Temeke(Keko), Kinondoni(Magomeni).
Halmashauri nyingine ni pamoja na Kasulu (kata ya Kitanga), Kasulu Mji( Kata za Kigondo na
Msambara), Buhigwe(Mnyegera), Bukoba(Buhendagabo, Nyakato, Kikomelo),
Misenyi(Kanyigo), Ngara(Nyamiaga), Mbinga(Utiri), Songea(Mpitimbi), Mbozi(Ilolo, Hasanga, Ihanda), Tandahimba(Nahyanga,
Namikupa), Dodoma(Dodoma Makulu), Serengeti(Geitasamo), Bariadi(Nkundwabiye) na Bariadi Mji(Nyangokolwa).
No comments:
Post a Comment