HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 07, 2018

WAZIRI UMMY AZINDUA DAWATI LA JINSIA, UANZISHWAJI WA MTANDAO WA WANAWAKE NA UTAMBULISHO WA SERA YA HAKI NA ULINZI WA MTOTO KATIKA JESHI LA MAGEREZA

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (katikati), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili  kushoto), na Viongozi  Waandamizi  wa  Jeshi  la Magereza  wakikata utepe  kuashiria  Uzinduzi  wa  Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza. Uzinduzi huo umefanyika leo katika Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiangalia bidhaa zinazotengenezwa  na Jeshi la Magereza  wakati alipotembelea mabanda ya jeshi hilo wakati wa Uzunduzi wa Dawati la Jinsia ndani ya Jeshi la Magereza lililozinduliwa katika Viwanja vya Karimjee, leo jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Serikali imesisitiza uwepo wa usawa wa kijinsia katika sekta mbalimbali ili kuendelea kuunga jitihada za kuwezesha usawa huo ambao uliasisiwa katika Mkutano wa Nne wa Dunia wa Wanawake uliofanyika Beijing nchini China mwaka 1995 huku ikisisitiza ni muhimu kuundwa kwa madawati ya jinsia katika idara za serikali.
Hayo yamesemwa na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizindua   Mtandao  wa  Wanawake  na  Utambulisho  wa Sera ya Haki na Ulinzi wa Mtoto katika Jeshi la Magereza leo  jijini Dar es Salaam .
Amesema Serikali imeweka mkazo katika kuhakikisha usawa wa kijnsia unafikiwa katika sekta na nyanja mbalimbali kwa kuchukua hatua ikiwemo kuandaliwa kwa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia ya mwaka 2000 pamoja na Mkakati wa Utekelezaji wake kwa lengo la kuweka mazingira muafaka na kuhakikisha kuwa masuala ya jinsia yanzingatiwa na wadau ikiwemo Wizara, Idara na Wakala  za Serikali, Mamlaka  za Serikali za Mitaa, Sekretarieti za Mikoa, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na Wadau wa Maendeleo.
“Leo nimefarijika  kuzindua dawati la jinsia katika Jeshi la Magereza ni hatua nzuri kuelekea lengo la serikali kuhakikisha usawa wa kijinsia unakuwepo na kulinda haki za watoto, ni tumaini langu taasisi zingine zitaiga mfano huu ili tuweze kufikia dhumuni la serikali ya Awamu ya Tano kuona usawa wa kijinsia unakuwepo” alisema Waziri Ummy
Akizungumza katika Uzinduzi huo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni aliwataka waratibu wa dawati hilo kuhakikisha wanasimamia haki hasa katika mashauri yanayowahusisha watoto na wanawake wajawazito waliopo magerezani na kuhakikisha ushirikiano unakuwepo kati ya wadau mbalimbali kuhusu ukaaji wa watoto magerezani
Pia amewataka viongozi wa Jeshi la Magereza kuhakikisha dawati hilo la jinsia linakua imara na madhubuti kwa kuweza kupata mafunzo mbalimbali yanayohusu haki za motto aliyepo gerezani na akiahidi wao kama wizara kuhakikisha dawati hilo linadumu na kuweza kutoa matunda mazuri.

No comments:

Post a Comment

Pages