Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi
ya Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, kwenye Makazi ya Waziri
Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 24, 2019.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa
katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi
katika Utumishi wa Ummam, kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jiji Dar es
salaam, Januari 24, 2019. Kutoka kushoto ni Mwanasheria wa Bodi, Dkt.
Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro, Mwenyekiti wa
Bodi, Donald Ndagula, Mjumbe wa Bodi, George Mlawa na Katibu Mtendaji wa
Tume, Mariam Mwaniulwa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Bodi ya
Mishahara na Maslahi katika Utumishi wa Umma, George Mlawa baada ya
mazungumzo na wajumbe wa Bodi hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu jijini
Dar es salaam, Januari 24, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mwanasheria
wa Bodi, Dkt. Charles Kato, Katibu Msaidizi wa Bodi, Fortatus Mbiro,
Mwenyekiti wa Bodi, Donald Ndagula na Katibu Mtendaji wa Tume, Mariam
Mwaniulwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana
na kufanya mazungumzo wa wajumbe wa Bodi ya Mishahara na Maslahi katika
Utumishi wa Umma na ameitaka ifanye kazi kwa weledi.
Ameiagiza
ifanye marekebisho ya maslahi kulingana na mazingira ya mtumishi,
akitolea mfano kada za elimu, afya, kilimo na mifugo ili yalingane na
kazi wanazozifanya.
Amekutana
na wajumbe wa bodi hiyo leo (Alhamisi,Januari 24, 2019) katika kikao
kilichofanyika kwenye makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Waziri
Mkuu amesema Serikali ina nia njema ya kuhakikisha mishara na maslahi
ya watumishi wa umma nchini yanaboreshwa, hivyo ameiagiza bodi hiyo
ifanye kazi kwa bidii.
Amesema
Serikali imeunda bodi hiyo ili kupata ushauri utakaotokana na tathmini
sahihi ya nini Serikali inatakakiwa kufanya ili kuboresha utendaji wa
watumishi wa umma nchini.
Serikali inaimani kubwa na wajumbe wote wa bodi hiyo kutokana na uzoefu walionao kwenye utumishi wa umma.
“Tunataka
muongozo mzuri wa kuwafanya watumishi wa umma wafanye kazi yao kwa
waledi bila ya kuwa na vishawishi vya aina yoyote ikiwemo kuomba na
kupokea rushwa.”
Amesema
Serikali inataka kila mtumishi wa umma anawajibika ipasavyo katika
kuwatumikia wananchi mambo ambayo yatakuwa yameimarishwa kutokana na
upatikanaji wa maslahi mazuri.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980
41193 –Dodoma,
ALHAMISI, JANUARI 24, 2019.
No comments:
Post a Comment