Daktari Bingwa wa Kina mama, Dk. Geofrey Marandu, akichangia mada katika mkutano uliowakutanisha madaktari bingwa wa Muhimbili kuhusu namna bora ya kuboresha huduma za matibabu katika hospitali hiyo. (Picha na John Stephen-MNH).
Na Mwandishi Wetu
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesema unaangalia jinsi ya kuboresha mfumo wa kliniki ili wagonjwa wahudumiwe kwa wakati baada ya kufika katika hospitali hiyo kupata huduma za matibabu.
Na Mwandishi Wetu
Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesema unaangalia jinsi ya kuboresha mfumo wa kliniki ili wagonjwa wahudumiwe kwa wakati baada ya kufika katika hospitali hiyo kupata huduma za matibabu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru wakati akizungumza na madaktari
bingwa wa Muhimbili kuhusu namna bora kuboresha huduma za matibabu katika
hospitali hiyo.
Hospitali hiyo inahudumia
wagonjwa wa nje 1,500 kwa siku. Pia, kuna wagonjwa 1,200 hadi 1,300 wamelazwa
wodini wakati wote. Aidha wagonjwa wa nje walio wengi wanapenda kuja asubuhi
hata kama kliniki zao zinaanza mchana.
Prof. Museru amesema hatua hii ina lengo
la kuboresha huduma katika kliniki hizo ni kuondoa msongamano wakati
mgonjwa au wagonjwa wakisubiri kuona madaktari bingwa wa hospitali hiyo.
“Wakuu wa idara kupitia kwa madaktari
mtuletee mapendekezo ambayo tutaangalia jinsi ya kujenga mazingira bora ambayo
wagonjwa watatumia muda mfupi kumuona daktari. Tunataka mgonjwa asikae muda
mrefu kwenye foleni,”amesema Prof. Museru.
Pia, Prof. Museru amewaahidi wataalam hao
kwamba Uongozi wa Hospitali chini ya Bodi ya Wadhamini utaendelea kuboresha
mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma bora kwa wananchi mbalimbali
wanaofika hospitali hapo kupata matibabu.
“Naomba tuendelee kutumia vizuri na
kikamilifu miundombinu iliyopo ili kuongeza tija na wananchi wametuamini ndiyo
maana wengi wamekuwa na matumaini makubwa sana na huduma tunazotoa” alisema
Prof. Museru.
Prof. Museru amewashukuru sana watoa
huduma na wafanyakazi wote kwa ujumla wao kwa namna ambavyo wanajituma na
kufanya kazi kwa bidii hali iliyoifanya Hospitali kufanya mageuzi makubwa
katika utoaji wa huduma bora za afya hapa nchini hususani katika kipindi cha
miaka mitatu iliyopita.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa katika
hospitali hiyo, mkurugenzi huyo amesema licha ya dawa kupatikana kwa zaidi ya
asilimia 95 hospitali yake inaendelea kuimarisha utoaji wa dawa kwa
wagonjwa ili kuhakikisha kila mgonjwa anayetibiwa anapata dawa kwa wakati.
Katika mkutano huo madaktari walijadili
njia za kuimarisha utoaji wa huduma bora za matibabu kwa wagonjwa mbalimbali
samabamba na kukubaliana kufanya kazi kwa juhudi ili kufikia malengo yaliowekwa
na hospitali hiyo ya kutoa huduma bora za ubingwa wa juu nchini.
Hospitali ya Taifa Muhimbili ina
wafanyakazi 2,705, kati yao madaktari ni 328, ambapo madaktari bingwa ni 186 na
142 ni madaktari wa kawaida. Aidha, Hospitali ina wauguzi 946 na waliobaki ni
wafanyakazi wa kada nyingine.
No comments:
Post a Comment