Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR), Habibu Mchange, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2019.
Baadhi ya waandishi wa habari.
NA JANETH JOVIN
ASASI ya Kiraia inayojihusisha na masuala ya kijamii na utetezi wa haki za binadamu (ADOR) imesema kuwa muswada mpya wa sheria wa vyama vya siasa uliyotolewa hivi karibuni una lengo la kudhibiti kikamilifu fedha za ruzuku za vyama vya siasa.
Asasi hiyo pia imesema muswada huo kama utapitishwa na kuwa sheria rasmi, utadhibiti ukomo wa uongozi wa juu katika vyama vya siasa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa asasi hiyo, Habibu Mchange alisema kwa sasa baadhi ya vyama vya siasa vimekuwa vikilaumiwa juu ya matumizi mabaya ya fedha hivyo anaamini uwepo wa muswada huo ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria itadhibiti jambo hilo.
Alisema licha ya baadhi ya watu wakiwemo wanasiasa kuulalamikia muswada huo, yeye kama mwanademokrasia nchini anaamini kuwa sheria hiyo itasaidia kukuza na kuvijenga vyama vya siasa.
“Mimi na asasi yangu pamoja na vijana wenzangu tunamshukuru aliyependekeza muswada huu, kwani huko nyuma niliwahi kukandamizwa nikiwa katika vyama kutokana na kutokuwepo kwa sheria hii.
“Kupitia muswada huu ambao kama ukipitishwa utakuwa sheria utakwenda kusimamia vema ruzuku za kila chama cha siasa, kwani Sheria inaeleza kuwa Msajili wa vyama vya siasa atatoa ruzuku kwa vyama na kuelekeza namna ya kuzisimamia , nashangaa kwanini baadhi ya vyama vya upinzania vinapinga jambo hili,” alisema.
Alisema demokrasia ni kugombea nafasi na si watu kushikiria madaraka muda mrefu kwa kuwakandamiza wanasiasa waliopo hivyo kwa kupitia sheria hiyo itawafanya wanasiasa wote kuwa sawa.
“Kutungwa kwa muswada huu kutawasaidia wanasiasa wanaoumia ndani ya vyama vyao kuwa kitu kimoja na kuondoa ukilitimba na Umungu watu,” alisema na kuongeza kuwa
“Viongozi wa chama wengi wamekuwa wakijimilikisha vyama kwa kudai wanamichango mikubwa ndani ya vyama, sheria hii itaondoa jambo hilo na migogoro na kuwa sehemu ya kusimamia maendeleo ya nchi,” alisema.
Aidha alisema Muswada huo utampa nguvu Msajili wa Vyama vya Siasa kufanya kazi za wananchi ipasavyo pasipo kuingiliwa na chama chochote cha siasa.
“Ndani ya vyama vya siasa kuna watu ambao awapandi vyeo kila siku wana cheo kilekile, hii yote ni kutokana na uwepo wa mfumo usiokuwa bora wa chaguzi ndani ya chama,” alisema.
Hata hivyo, Mchange amewataka watanzania kutambua kuwa mabadiriko ya Katiba ni pamoja na mabadiriko ya sheria ndogo ndogo ikiwemo ya vyama vya siasa.
“Sheria itakayotungwa itawapa wanasiasa sehemu moja ya kulalamika na kuwaweka kati wanasiasa wote kwa kuongea lugha mojab,”alisema
Alisema Watanzania wanapaswa kufahamu muswaada huu unafaida kubwa kwa nchi kwani itasaidia kudhibiti fedha za ruzuku na kukuza vipawa kwa wanachama .
Wakati hayo yakielezwa tayari vyama 10 vya siasa nchini vimefungua kesi Mahakama Kuu ya kupinga muswada huo wa sheria ya vyama vya siasa nchini.
Kesi hiyo ilifunguliwa rasmi Disemba 20, mwaka jana na vyama hivyo vya upinzani vilivyoungana kupinga uamuzi huo wa serikali huku mshtakiwa mkuu akiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisoma tamko la vyama hivyo kwa waandishi wa habari na kusema kuwa mshtakiwa si Bunge.
Alisema lengo la muswada huo ni kuvikandamiza vyama vya siasa na kufanya shughuli zote za kisiasa kuwa jinai.
Alisema muswada huo unalenga kumfanya msajili kuwa mamlaka ya usimamizi wa vyama vya siasa na kuingilia shughuli za kiutawala na maamuzi ya ndani ya vyama kama kumsimamisha au kumfukuza uanachama mwanasiasa.
Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Novemba 16, mwaka jana na miongoni mwa mambo yanayopendekezwa ni kuongezwa kwa kifungu ambacho kitamwezesha Msajili wa Vyama vya Siasa kusitisha usajili wa chama cha siasa kitakachovunja masharti ya sheria.
Wakati wa kusomwa muswada huo, Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge, alisema Spika wa Bunge, Job Ndugai ataipangia Kamati ya Bunge itakayofanya uchambuzi.
Kilichopo kwenye Muswada
Miongoni mwa mambo yaliyo katika muswada huo ni Kifungu cha 19 kinapendekezwa kurekebishwa ili kumwezesha msajili wa vyama vya siasa kufuta usajili wa chama cha siasa kitakachobainika kuwa kilipata usajili kwa njia zisizo za halali.
Pia, muswada huo unalenga katika kuzuia viongozi wa vyama vya siasa kutokuwa wajumbe wa bodi ya wadhamini.
Muswada pia unapendekeza kufuta kifungu cha 21A na kifungu cha 21B kinapendekezwa kufanyiwa marekebisho ili kuliwezesha Baraza la Vyama vya Siasa kupata fedha kutoka katika bajeti ya Serikali na wafadhili.
Muswada huo unapendekeza pia kuongezwa kwa vifungu ili kuainisha makosa na adhabu na kusitishwa kwa usajili wa vyama vya siasa vitakavyokiuka masharti ya sheria.
Pia unapendekeza kufanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka waziri mwenye mamlaka ya kutengeneza kanuni za uandaaji wa taarifa za hesabu za vyama vya siasa na mambo yatakayojumuishwa katika katiba za vyama vya siasa.

No comments:
Post a Comment