HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 06, 2019

NSSF YAANZA KUTEKELEZA MAAGIZO YA MHE. RAIS

Meneja Kiongozi wa Matekelezo wa NSSF, Cosmas Sasi, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari 6, 2019 kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais kuhusu mafao mbalimbali kwa wanachama wake.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma NSSF, Lulu Mengele, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya Mh. Rais.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
 
Na Mwandishi Wetu
 
NSSF imeanza utekelezaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa katika mkutano Kati ya viongozi wa vyama vya vyafanyakazi, Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mfuko unaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi, kilimo n.k.

Madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake.

Akizungumza katika mkutano huo, Meneja Kiongozi wa Matekelezo 'Chief Manager Compliance and Data Management', Cosmas Sasi, alisema NSSF inaendelea kulipa mafao mbali mbali kwa wanachama wake kwa wakati.


 Kwa upande wa mafao ya uzeeni takribani shilingi bilioni 5 zimekuwa zinalipwa kila mwezi kwa wastaafu wetu kuanzia julai 2018. Kwa pensheni ya mwezi Desemba, 2018 kiasi cha shilingi Bilioni 4.83 bilioni kimeshalipwa kwa wastaafu 18,631 walikuwepo kwenye daftari Ia wastaafu.

Kwa upande wa malimbikizo ya Mafao hadi kufikia julai 2018 jumla ya shillingi bilioni 108 zilikuwa zinadaiwa kwenye Shirika, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 85 kimelipwa kwa wanachama waliokuwa na madai mbali mbali baada ya uhakiki kukamilika, kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 23 kitalipwa baada ya uhakiki unaondelea kukamilika.

Kwa upande wake, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma (Chief Manager Public Relations and Education) Bi. Lulu Mengele alisema Mfuko ulianza zoezi Ia kuhakiki wastaafu wake kuanzia tarehe 1.12.2018 na zoezi hili linaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara .Wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wanaombwa wafike kwenye ofisi zetu 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF. 


Wastaafu wanatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo picha, kitambulisho cha Taifa au cha mpiga kura pamoja na kadi ya benki. Malipo ya pensheni kwa wastaafu ambao hawatahakikiwa yatasitishwa mwishoni mwa mwezi wa Januari 2019.Malipo ya wastaafu yatafanyika moja kwa moja kwenye akaunti za wastaafu ili kumrahisishia mstaafu kupata malipo yake ya pensheni kwa haraka na bila usumbufuZoezi Ia uhakiki litakuwa endelevu ili kuboresha taarifa zi|izokuwepo kwenye daftari la wastaafu

Shirika linasisitiza kwa wafanyakazi na maoflsa utumishi kuhakikisha madai yanayoletwa kwenye Mfuko ni sahihi na mtu atakayebainika kuleta madai ya kugushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani kwani hilo ni kosa la jinai.

No comments:

Post a Comment

Pages