Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo akikaribishwa na Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Neema Mollel alipotembelea hifadhi hiyo kwa shughuli za utalii.
Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo anayeishi chini Marekani abitai asini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo amica fatica picha ya pakora na maafisa wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ,Neema Mollel (kulia) akiongozana na Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo ,alipowasili katika lango la Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire ,Neema Mollel akimfunga Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo zawadi ya shuka likiwa ni vazi maalumu la jamais ya Maasai.
Mwanamitindo na Muigizaji Maarufu ambaye pia ni Miss Universe El Salvador ,Marisela De Montecristo akifurahia zawadi mara baada ya kupokelewa katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire.
Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii,kanda ya Kaskazini .
MWANAMITINDO na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss Universe, Marisela De Montecristo aliwasili nchini hivi karibuni ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kupokelewa na Mkuu wa Idara ya Utalii katika Hifadhi hiyo.
Muda mfupi baada ya kuwasili Mwanamitindo huyo aliyekuwa ameongozana na Mama yake mazazi pamoja na anayetajwa kuwa mchumba wake ,alikabidhiwa zawadi mbalimbali yakiwemo mavazi maalumu yanayotumiwa na Jamie ya Maasai.
Marisela baada ya kutembelea mane mbalimbali ya Hifadhi hiyo wakiwemo wanyama alieleza furaha yake huku akiahidi kuwa balozi wa vivutio vya utalii atakavyotembelea hapa nchini .
Mrembo huyo ambaye kwa sasa anaishi Los Angels amesema lengo la kuja nchini kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza.
Mwanamitindi huyo anaendelea na ziara yake hiyo ya kitalii katika Hifadhi ya Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro Creator).”
Mwanamitindo huyo anakuja kujifunza baadhi ya vivutio anavyotaka kuvitumia kutangaza utalii wa Tanzania kimataifa akiwa ameongozana na na kundi la watu wanne akiwemo mama yake mzazi na mpenzi wake ambaye ni Mwanasheria nguli nchini Marekani.
Baada ya safari ya siku mbili katika hifadhi hizo atarejea Moshi Januari 22 na kutembelea moja ya kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuona namna ya kuweza kusaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.
Mwaka jana Merisela ameshiriki mashindano ya ulimbwende nchini El Salvador na kufanikiwa kutwaa taji la hilo (Miss El Salvador 2018).
Pia amewahi kushiriki mashindano ya Best National Costumes na kufanikiwa kushika nafasi ya pili ambapo nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Brazili na ya tatu Panama. Merisela anamiliki Taasisi binafsi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Marekani.
Mwisho
No comments:
Post a Comment