NA MWANDISHI WETU
BENKI ya NMB, imesema inatambua umuhimu wa elimu na afya kwa Watanzania, hivyo itaendelea kusaidia katika sekta hizo, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwahudumia wananchi wake.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Meneja wa NMB Kanda ya Nyanda za Juu, Straton Chilongola, wakati akikabidhi msaada wa madawati 102 kwa shule za Msingi Mwasanga na Hekima za Jijini Mbeya.
Sanjari na hilo, NMB imekabidhi jumla ya mabati 324 kwa shule za Msingi Mlima Reli ya Wilaya Mbeya na Mapinduzi ya Jijini Mbeya na vitanda, magodoro na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi vyote vikiwa na thamani ya milioni Sh. 25.
Chilongola alisema NMB ni wadau muhimu kwa Serikali na Watanzania, hivyo wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo kwa sababu jamii wanayoisaidia ndiyo inayowawezesha kupata faida katika biashara yao.
“Tunambatua changamoto ya elimu na afya, sisi NMB tunazipa kipaumbele sana kwa sababu hizi sekta mbili ni muhimu mno katika ustawi wa jamii yetu,” alisema Chilongola.
Chilongola alisema katika kipindi cha mwaka huu wa 2019, NMB imetenga Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii, ikiwamo skta za afya, elimu na yanapotokea majanga kwa nchi nzima.
Awali, Mwalimu Mkuu wa Shule Msingi Mwasanga, Keneth Amon, alisema shule yake inakabiliwa na msongamano wa mkubwa wa wanafunzi madarasani kutokana uhaba wa wa vyumba vya madarasa, upungufu wa madawati.
Alisema: “Msongamano ni mkubwa sana darasani, shule nzima tuna madawati 237, lakini kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi, tunakabiliwa na upungufu wa madawati 140, vile vile tuna upungufu wa ofisi za walimu.
“Shule ina walimu 22 na wote tunatumia ofisi moja ambayo nayo ni finyu mno jambo ambalo kwa kweli inatuwia vigumu kumudu majukumu ya kila siku,” aliasema Amon.
Akizungumza na baada ya kupokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, alisema NMB inatambua umuhimu wa kusaidia jamii kama walivyofanya, ikitambua kwamba Serikali pekee haiwezi kufanya kila jambo kwa wananchi wake licha ya kuwa ndio wajibu wake.
Alisema: “Niwaombe wazazi kwamba shule zimeshafunguliwa sasa hivyo asiwepo mwanafunzi ambaye hafiki shuleni, na nyinyi wanafunzi hakikisheni mnatunza madawati haya na msome kwa bidii.
“Leo NMB imetambua umuhimu wa elimu bora kwa kuwatengenezea mazingira bora ya kusomea na ndiyo maana imeleta madawatin haya’.
Ntinika amefafanua kuwa mahitaji ya huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu yanahitaji kuungwa mkono na taasisi na mashirika mbalimbali ya kijamii kama ilivyofanywa na NMB ambayo imechangia vitanda na mashuka kwa Hospitali Teule ya Mbalizi.
No comments:
Post a Comment