HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 31, 2019

Vicky Ibrahim aibuka kidedea ‘Wakala Chief Promotion’


Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed, akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwakabidhi zawadi mawakala wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 iliyojulikana kama ‘Wakala Chief Promotion’  (Na Mpiga Picha Wetu).
Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu, James Sumari, akiwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania.
Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed, akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya Sh. Mil. 20, wakala wa kampuni hiyo, Vicky Ibrahim,  katika hafla ya kuwakabidhi zawadi mawakala wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 iliyojulikana kama ‘Wakala Chief Promotion’. 
Baadhi ya washindi wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed (katikati).
 
Na Costancia Nkindi

KAMPUNI ya Tigo Tanzania, imetoa zawadi ya fedha taslimu kwa mawakala wake wa Tigo Pesa waliofanya vizuri katika promosheni ya mwisho wa mwaka 2018 inayojulikana kama ‘Wakala Chief Promotion’.


Kupitia promosheni hiyo, wakala aliyefanya vizuri kuliko wote nchini, amepokea zawadi ya fedha taslimu Sh. Milioni 20 wakati mawakala wengine wanaofuatia kwa kufanya vizuri kutoka kanda nne wakipokea jumla ya Sh. Milioni 40.


Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuwakabidhi washindi zawadi zao, Mkuu wa Huduma za Kifedha wa Tigo, Hussein Sayed, alisema promosheni hiyo imewekwa maalum kwa ajili ya kuwashukuru na kuwazadia mawakala wanaofanya vizuri katika kipindi cha mwisho wa mwaka.


Hussein, alisema washindi 20 kutoka kanda nne ambazo ni Pwani, Kusini, Kaskazini na Kanda ya Ziwa walipatikana, ambapo kila kanda ilitoa washindi watano ambao kila mmoja alijinyakulia zawadi ya Sh. Milioni 2 wakati mshindi wa jumla akiondoka na Sh. Milioni 20.


“Jumla ya mawakala 90,000 walishiriki katika promosheni hii ya nchi zima iliyoanza tarehe 1 Disemba na kumalizika tarehe 31 Disemba 2018,” alisema.


Kwa upande wake Mkuu wa Bidhaa Huduma za Kifedha kwa njia ya Simu, James Sumari, aliwashukuru Mawakala kwa mchango wao mkubwa katika kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania


Naye Vicky Ibrahim, ambaye ni mshindi mkubwa katika promosheni hiyo kutoka Kanda ya Pwani Mkoa wa Dar es Salaam, alisema Sh. Milioni 20 alizojishindia zitamsaidia kupanua biashara yake hiyo ya Tigo Pesa huku akiishukuru kampuni ya Tigo kwa zawadi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages