HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2019

WAKULIMA KUSAJILIWA NA KUPATIWA VITAMBULISHO NCHINI

 Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa salamu za mkoa huo wakati wa mkutano wa kitaifa wa siku moja wa  wadau wa Tumbaku nchini uliofanyika leo.

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga akifungua  mkutano wa kitaifa wa wadau wa Tumbaku nchini uliofanyika jana mkoani Tabora uliokuwa ukijadilia masuala mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalishaji. Picha na Tiganya Vincent.

NA TIGANYA VINCENT, TABORA

SERIKALI imeziagiza Bodi zote zilizoko chini ya Wizara ya Kilimo kuanza mara usajili wa wakulima wa mazao yote na zihakikishe zinawapa vitambulisho kwa ajili ya kuwatambua na wanapofanyika kazi zao ili iwe rahisi kuwahuduma.

Hatua hii inalenga kuwatambua na kuwasaidia kuboresha kilimo chao ili waweze kupata huduma za uhakika kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga wakati akifungua mkutanowa kitaifa wa mwaka wa wadau wa sekta ya Tumbaku Tanzania.

Alisema hatua inalenga kuwatambua wakulima wote na maeneo ambayo wanalima ili kuwaondoa na kilimo cha kujikimu na kuelekea katika kilimo cha kibiashara na kisasa.

Hasunga alisema hadi hivi sasa ni Bodi ya Tumbaku pekee ndio imesajili wakulima na kuwapa vitambulisho.

“Lazima tuanze kuwatambua wakulima wetu walipo, mashamba wanayolima na ukubwa wake na mazao wanayolima na kiwango mazao ambacho wanatarajia kuzalisha ” alisisitiza.

Hasunga alisema lazima shughuli ya kilimo ianzie kutambulika kama zilivotaaluma nyingine.

Alisema kukosekana kwa takwimu halisi za wakulima , ukubwa wa mashamba yao na walipo kumesababisha kuwa vigumu huduma muhimu kwa ajili ya kuboresha kilimo kuwafikia na kusababisha wapatiwe huduma za kitaaalamiu ambao halizingani na mahitaji yao na wakati mwingine sio halisi.

Waziri hiyo wa Kilimo aliongeza kuwa nguvu kubwa lazima ielekezwe katika kuwasaidia wakulima kulima cha kisasa kwa sababu ndicho kinatoa ajira kubwa kwa Watanzania ambapo asilimia 65 ya wananchi wamejiari katika kilimo na asilimia 8 wanashughulika na biashara inayotokana na mazao ya kilimo.

Katika hatua nyingine Hasunga amegiza Bodi ya Tumbaku Nchini na wadau wa zao hilo kuhakikisha wanasaidia kuinua zao la Tumbaku ambalo limeshuka na kupoteza uongozi wa kuwa zao linaloingiza fedha nyingi za kigeni.

Alisema uzalishaji umeshuka kutoka tani 126,000 kwa msimu wa mwaka 2010/11  hadi kufikia tani 54,800 kwa msimu 2018/19 na kuongeza kuwa hata wastani wa bei umeshuka kutoka wastani wa Dola 2.11   kwa msimu wa mwaka 201/11 na kufikia Dola 1.72 mwaka 2018/19.

Hasunga alisema ni lazima Bodi ya tumbaku na wadau wengine kuja na mikakati ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo ambalo siku za nyuma lilikuwa likiongoza kuingiza fedha za kigeni nchini.

Alitaja mikakati ni pamoja na kutafuta wanunuzi wengine sehemu mbalimbali ili kuongeza ushindani wa bei na kumnufaisha mkulima na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania Hassan Wakasuvi alisema kuwa moja ya mambo ambayo yatawezesha kuleta mabadiliko katika sekta ya tumbaku ni marekebisho ya Sheria ya tumbaku.

Aliwataka wadau kuwa tayari kutoa maoni yao wakati ukiwaidia ili kuwepo na Sheria nzuri.

No comments:

Post a Comment

Pages