Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wilayani Mkinga, wakati wa kikao kazi
cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao
chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani humo. (Picha na Ofisi ya Rais-Utumishi).
Baadhi ya watumishi
wa umma wilayani Mkinga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo
pichani) wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi
hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani humo.
Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Katibu
Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said, kabla ya kuzungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao,
kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF
wilayani humo.
Katibu Tawala
Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga (hawapo pichani) wakati
wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF wilayani humo.
Afisa Utumishi Mwandamizi
wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.
Baraka N. Nangosongo akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa
umma wilayani Mkinga wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla kukagua utekelezaji
wa miradi ya TASAF wilayani humo.
No comments:
Post a Comment