Mbunge
wa
Geita mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhe.Constantine
Kanyasu ameomba umeme kupitia mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini
wa REA
katika jimbo la Geita mjini kutokana na sababu kuwa Geita mjini, mjini
ni kata mbili tu ikiwemo Kalangalala, Bombambili na maeneo
yote yaliyobaki ni vijiji.
Pia,
Mhe.Kanyasu amemuomba Waziri wa Nishati, Dkt.Medald Kalemani kuharakisha zoezi
la usambazaji wa umeme wa REA katika maeneo ya
yaliyoyopitiwa na umeme huo kwa vile tokea mradi huo ulipozinduliwa
mwaka jana, kijiji kimoja tu katika
jimbo hilo ndo kimenufaika na mradi huo.
Kauli
hiyo imetolewa na Mbunge huyo wakati wa uzinduzi wa umeme wa REA
uliofanyika katika kijiji cha ibanda katika wilaya ya Geita mkoani
Geita, eneo ambalo linalohesabika kuwa ni mtaa.
Akizungumza
kabla ya kuzindua umeme huo, Dkt.Meldard Kalemani ametaja sababu zilizoifanya Geita mjini kuchelewa kupata
umeme wa REA kwa vile Geita mjini inahesabika kuwa ni mjini na mjini hakuna vijiji bali kuna mitaa.
"Sisi
tuliambiwa tupeleke umeme kwenye vijiji na sio kwenye mitaa, Mhe. Kanyasu ndo
kapigania kutuambia kuwa hii sio mitaa bali ni vijiji" Amesisitiza Waziri
Kalemani
Hata hivyo,
Waziri Kalemani amemhakikishia Mbunge wa Geita mjini kuwa jumla ya vijiji 42 tayari
vipo kwenye mpango wa kuunganishwa na mradi wa umeme wa REA.
Katika hatua
nyingine, Waziri Kalemani amewaagiza
Wakandarasi na Wataalamu wote kuwa hakuna kuruka nyumba wala kubagua
nyumba wahakikishe kila mhitaji anaunganishiwa umeme haraka iwezekanavyo.
Aidha, Waziri
Kalemani amepiga marufuku kuwatoza wananchi wanaotaka kuunganishiwa umeme zaidi
ya shilingi 27,000/- na kutoa wito kwa mwananchi atayetozwa zaidi ya kiasi
hicho atoe taarifa ili hatua kali dhidi ya wahusika ziweze kuchukiwa.
Aidha ametoa
wito kwa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ya kuunganishiwa kwa gharama hizo
kwani baada ya hapo itabidi walipie kulingana na taratibu za Shirilka la Ugavi
wa umeme Tanzania(TANESCO
No comments:
Post a Comment