Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), juu ya kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), juu ya kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Tanzania na
Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya
udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa
yote nchini iliyopo mipakani
Hayo yamebainishwa na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa
mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni
mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa
ya mipakani
“Kama Serikali tuna
vipaumbele katika kudhibiti mipaka yetu kutokana
na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu,
uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana
tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu
huo”alisema Masauni
Akizungumza katika
kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania
ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti wa mipaka.
“Tuna uhusiano mzuri
baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza
kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa
mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak
Katika mazungumzo hayo
pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali
ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika
shughuli za uokozi.
No comments:
Post a Comment