Vijana wa Chama cha Wananchi CUF, (JUVICUF) wamemuambia Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kuwashushia msimamo wa chama dhidi ya mgogoro uliopo wakidai kuwa sasa wanataka kulinda chama chao na kukiona kinaimarika.
Akizungumza katika mkutano maalumu wa kula kiapo cha utifu dhidi viongozi wa CUF Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya hiyo, Abeid Khamis Bakar, alieleza kuwa sasa ni muda muwafaka kwa vijana kuchukuwa nafasi yao ya ulinzi na uimarishaji wa chama hicho.
“Mh. Katibu Mkuu hili ni jeshi lako ambalo linasubiri amri tuu kutoka kwako liaze kazi kwani muda wa sasa si wakuchezewa na mtu yeyote” alieleza Bakari.
Kaimu huyo alieleza kuwa wakotayari kukilinda chama chao kwa gharama yoyote kutokana kubeba imani ya umma mkubwa wa Watanzania.
Kwa upande wake Maalim Seif aliwataka vijana wamstahamilie kwa muda mfupi tuu na lolote litakalo amuliwa kwa ajili ya chama litashushwa kwao.
Alisema wanachosubiri ni hukumu za kesi zao mbili ziliopo Mahakamani ya tarehe 18 na 22 mwezi huu zitolewe hukumu na baada ya hapo watashusha kazi kwa ngazi zote za chama.
“Mimi natembea kifua mbele kwa sababu nina jeshi kubwa ambalo halina hata bunduki, vijana wangu nukuaminini sana lakini tusubiri kidogo” alieleza Maalim Seif.
Alisema vijana wanandamwa ili CUF iondoke nia ya Rais magufuli sio CUF kuondoka lakini kiwe ni chama dhaifu kinachosubiri amri kutoka CCM kwani ndio sababu ya Lipumba katumwa kwenda kuvuruga katika chama cha CUF kwa kile alichodai wakati mwanzo alijiuzulu ndio mana jitihada za kuungwa mkono na serikali ili watimize azma yao.
Nae mwenyekiti wa Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wa JUVICUF Bobali alisema maendeleo ya vitu hayana thamani kama watu wake hawana uhuru na vijana Tanzania bado hawajapata uhuru wa kweli kutokana kile alichodai utawala mbovu wa Chama cha Mapinduzi
Hivyo amewataka vijana kutembea kifua mbele na kuendelea kumunga mkono Katibu wao mkuu Malim Seif Sharif kwani ana dhamira ya dhati ya kuikomboa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake.
No comments:
Post a Comment