Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (katikati) akipata
maelezo namna ujenzi wa Ofisi za Wizara unavyoendelea kutoka kwa
Mhandisi Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
alipotembelea eneo la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini
Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (watatu kulia) akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bi. Grace Sheshui (wakwanza kulia), wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akisaini kitabu cha wageni alipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango
(kushoto) akioneshwa ramani ya majengo Wizara hiyo kutoka kwa Mhandisi
Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alipotembelea eneo
la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali- WFM)
Na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango.
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mh. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema ameridhishwa na kasi ya
ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango zinazojengwa katika Mji wa
Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Mh. Mpango ameyasema
hayo leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo ambazo
zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
‘Nafikiri tunaenda
vizuri, quality of work inanifurahisha,
ikifika tarehe 1 Machi, 2019, nijisikie
nipo huru sasa nabadilisha ofisi nipo Ihumwa’ alisema .
Aidha Dkt. Mpango
ameuagiza Uongozi wa Wizara kuanza mchakato wa ujenzi wa Jengo kubwa la Ofisi
ili kuweza kutosheleza Watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Kwa upande wake Msimamizi
wa ujenzi wa Ofisi hizo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi
Elisante Ulomi amesema ujenzi wa awamu ya kwanza umejumuisha Ofisi ya
Mh.Waziri, Mh. Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Wakuu, ukumbi wa
mikutano, ofisi za madereva, pamoja na ofisi za Wakurugenzi saba.
Mhandisi Ulomi
amesema ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 92, na utakamilika tarehe 28
Februari,2019.
No comments:
Post a Comment