Wakazi wa vijiji vya
kisanga,kata ya talawanda katika halmashauri ya chalinze mkoani pwani
wametakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na vyoo bora.
Mtendeji wa kijiji cha kisanga Exaud Edward mhelela akitoa ufafanuzi wa jinsi ya kuwa na vyoo bora
NA FREDY MGUNDA, PWANI
WAKAZI wa vijiji vya kisanga,kata ya talawanda
katika halmashauri ya chalinze mkoani pwani wametakiwa kujenga utamaduni wa
kuwa na vyoo bora ilikuepukana na magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na kula
kinyesi cha binadamu.
Akizungumza na wakazi wa vijiji
hivyo wakatika wa kampeni ya uhamasishaji wa ujenzi wa vyoo bora,mtendeji wa
kijiji cha kisanga Exaud Edward mhelela,alisema ni muhimu kwa kila kaya
kuhakikisha inakuwa na chuo safi na bora watakachotumia kwa ajili ya
kujisitili.
Amesema kila kaya inatakiwa
kuwa na chuo bora na safi kwa ajiri ya familia yake,kwani magonjwa mengi ya
mlipuko husababishwa na watu kula kinyesi cha binadamu na endapo kutakuwa na
magonjwa ya mlipuko ya mara kwa mara,basi yatasababisha kupunguza nguvu kazi ya
taifa na maendeleo kurudi nyuma.
“ndugu zangu maendeleo yoyote
hayawezi kuja katika kijiji chetu cha kisanga bila kuwa na maji safi,mazingira
na rafiki ikiwemo (vyoo),hivyo ni muhimu tutahidi katika uhamasishaji wa kuwa
na vyoo safi na bora kwa kila kata” alisema.
Kwa upande afisa mradi wa WARIDI,Samson
Mbwasi alisema hali ya usafi na mazingira katika vijiji vya kisanga na Msigi
ilikuwa sio nzuri kwa sababu kaya nyingi zilikuwa hazina vyoo bora.
Alisema mara baada ya kuingia
kwa mradi huo wa PDF/WARIDI Chalinze na kuwapatia mafunzo watendaji wote wa
vijiji,walikusanya taarifa za usafi wa mazingira na imesaidia wananchi wengi
kujenga vyoo bora.
Alisema uongozi wa kijiji
ukiongozwa na mtendaji wa kijiji,waliwahimiza wananchi na kwapamoja
walikubariana kuboresha hali zao za usafi hususani kwenye ujenzi na matumizi
sahihi ya vyoo.
Alisema katika vijiji vyote
viwili vya kisanga na msigi,wamefanikiwa kuhamasisha ujenzi wa vyoo katika kaya
hamsini na nane (58) kati ya mia moja tisini na saba (197) sawa na asilimia 29.9.
No comments:
Post a Comment