HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 13, 2019

KAMPUNI YA MARCEDES-BENZ YAZINDUA MAGARI MAPYA

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Utengenezaji wa magari ya Mercedes-Benz imezindua magari mapya maroli aina ya Actros na Arocs februari 8 jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo wa malori wa kustajaabisha zaidi katika kanda ya Afrika Mercedes-Benz imepania kupeleka mbele historia ya malori yenye nguvu nchini Tanzania, ni malori ya kuaminika na yenye ufanisi kwaajili ya masafa marefu.

Akizungumzakatika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi wa Mauzo na Huduma kwa Wateja wa Malori ya Mercedes Benz Afrika, Torsten Bauerheim, alisema, malori yote mapya yametengenezwa katika mifumo ya kisasa na yenye kuhimili kila mazingira.

“Malori yote mapya ya Actros na Acros yanakuja na injini yenye ufanisi yenye silinda 6 katika mstari, vyumba vya dereva vya kisasa vinavyoruhusu hewa kupita na Mercedes PowerShift 3 ya kisasa, injini ya kujiendesha yenyewe zikiwa na miundo mbalimbali tofauti kutegemeana na mazingira ya kanda husika. 

“Malori yote mapya ya Actros ni ya kuaminika na ya uhakika kwaajili ya ujenzi na matumizi katika barabara za vumbi na zote zimepitia majaribio makali ya ubora ya zaidi ya kilomitea milioni 60 kabla ya kufanya uzinduzi wa masoko,”alisema Bauerheim

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa wasambazaji walioithibishwa wa Mercedes-Benz, CFAO Motors Tanzania, Marius Prinsloo, alisema Malori mapya ya Actros na Arocs yanatoa kiwango cha ziada cha uimara, ufanisi katika matoleo ya malori ya Mercedes-Benz.

“Yakiwa yametengenezwa katika kiwanda cha malori kikubwa kuliko vyote duniani nchini Ujerumani, Malori haya yanakuja katika aina mbalimbali mahususi kwaajili ya soko letu la Tanzania yakiwa yamebuniwa na kutengenezwa kuhimili mazingira magumu ya uendeshaji.

“Yamejaribiwa kwa kina duniani kote, katika barabara za aina zote na katika mazingira magumu zaidi, magari haya ni mifumo bora zaidi kwaajili ya kazi ngumu. Majaribio yalijumuisha jumla ya zaidi ya kilometa milioni 6 za mbio za ustahimilivu zilizofanywa na kituo cha majaribio ya malori ya Mercedes-Benznchini Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu,”alisema Prinsloo na kuongeza kuwa.

“Chumba kipya cha pekee cha dereva kimetengenezwa kwa kiwango cha juu cha vifaa na mazingira mazuri ya ndani, wakati uendeshaji ni rahisi na wakustarehesha . Aina zote mbili za malori ya Actros na Arocs zinavutia kwa teknolojia ya kisasa zaidi na mfumo wa kuaminika wa uendeshaji kutokea chanzo kimoja.

“Injini zenye ustahimilivu, zenye nguvu na zenye ufanisi zinapatikana katika aina za utoaji moshi wa Euro III, IV na V, ikiwa inatoa aina mbalimbali za nguvu ya msukumo kuanzia 240 kW (326 hp) mpaka 460 kW (625 hp). Ikiwa imeunganishwa na toleo la hivi karibuni la Mercedes PowerShift 3, gia boksi ya kujiendesha yenyewe, malori ya Actros na Arocs yanafikia kiwango cha juu cha ufanisi wa mafuta, ikiwa inachangia kuongeza faida za uendeshaji ,”alisema

Actros mpya zimetengenezwa kwaajili ya usafirishaji wa masafa marefu pamoja na usambazaji wa mizigo mizito. Zinapatikana kwa aina 22 tofauti za chumba cha dereva na zinakuja katika matoleo ya chuma au ya kushikiliwa na upepo.

Kwaajili ya mazingira magumu ya uendeshaji, Actros zinapatikana katika injini zenye nguvu za 15.61 na kasi ya 16 na gia boksi ya kujiendesha yenyewe ya Mercedes PowerShift 3

lakini pia alieleza kuwa Arocs mpya ya kustaajabisha imetengenezwa kwa ustadi wa kipekee iwe katika shughuli za ujenzi mbali mbali na barabara za lami.

Malori hayo ya  Arocs yanaelezwa kuwa yenye ustahimilivu mkubwa na uwezo wa kufanya kufanya kazi katika mazingira magumu zaidi ya barabara za vumbi mbali na bara bara za lami. Arocs zinapatikana kama Chassis-, Mixer-, Tipper- na aina mbalimbali za uendeshaji - kuanzia miundo ya 4x2 mpaka 8x8 na uzito (GCW) wa mpaka kufika tani 250.

Pia Maroli hayo yamewekewa viwango vipya pale inapokuja kuhusu suala la usalama na mifumo ya usaidizi, inayomsaidia dereva na kuokoa maisha.

No comments:

Post a Comment

Pages