Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kuhusu huduma za mahala
pamoja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wawekezaji Bi Anna Lyimo, Waziri
Kairuki alifanya ziara kwenye ofizi za TIC leo February 20, 2019.
Mkurugenzi Mtendahi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki alipotembelea kwenye ofisi hizo leo
February 20, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akitoa ufafanuzi wa jambo alipotembelea kwenye
ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Mapema February 20, 2019 ili kujionea
baadhi ya kazi zinazofanywa na kituo hicho sehemu ya huduma za mahala pamoja
Na Grace Semfuko-MAELEZO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji ) Angela Kairuki amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kupitia
mfumo wa huduma za mfumo wa mahala pamoja kuboresha utoaji wa huduma kwa
wawekezaji kupitia mfumo wa kielektroniki na kuwaagiza kuunganisha mfumo wa
dirisha la uchakataji miradi (TIW) kwenye Kanda zote saba za kituo hicho Nchini
ili kurahisisha mwenendo wa upatikanaji wa huduma kwa wawekezaji.
Kairuki alisema mfumo huo unasaidia
kuondokana na urasimu,ucheleweshwaji na unarahisisha upatikanaji wa
leseni,cheti na vibali ambao utasaidia
kuongeza wawekezaji nchini ambapo kati ya kanda saba za TIC ni kanda moja tu ya
Kaskazini ndio iliyoingizwa kwenye mfumo na kuagizwa kanda zingine ziharakishe
mfumo huo ndani ya mwezi mmoja.
Waziri Kairuki aliyasema hayo
February 20, 2019, baada ya kuzungumza na maafisa wanaotoa huduma ndani ya
mfumo wa mahala pamoja na kufanya nao majadiliano juu ya namna ya kuboresha
huduma hizo ambazo zinatolewa na taasisi 11 ndani ya jengo la TIC.
“Mfumo wa huduma za mahala pamoja ni mzuri
sana, lakini tuhahitaji kuyafanyia kazi masuala kadhaa kwenye kila taasisi 11
zilizopo kwenye huduma za mahala pamoja ili kuondokana na changamoto ambazo
zinachelewesha upatikanaji wa huduma za uwekezaji” alisema Kairuki.
Aidha aliwataka watendaji wa
ardhi ndani ya kituo hicho kuweka vizuri takwimu za ardhi ya uwekezaji na
kushughulikia changamoto za upatikanaji wa ardhi kwa wawekezaji ambao
unasimamiwa na TIC.
Akiwa katika sehemu ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania TRA Waziri Kairuki aliagiza watendaji hao kuuona umuhimu wa utoaji wa
cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi TIN kwenye Kituo hicho ili kurahisisha huduma
kwa wawekezaji.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji
Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe alisema iwapo Serikali itawezesha taasisi zote
zinazohusika na huduma za mahala pamoja kutoa huduma zake stahiki zinazohusu
uwekezaji ndani ya ofisi za TIC itakuwa ni hatua kubwa katika uwekezaji.
“Taasisi zilizopo ndani ya mfumo
wa mahala pamoja zinafanya kazi kubwa, tunachoomba sisi kama TIC ni kwamba
huduma za taasisi hizo kwa wawekezaji zikamilike ndani ya TIC badala ya kwenda
kwenye makao makuu ya ofisi hizo kufuata idhini ya vibali,leseni na vyeti
husika kwa wawekezaji” alisema Mwambe.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wawekezaji
Anna Lyimo alisema kwa sasa huduma za mahala pamoja zimekuwa na manufaa makubwa
kwa wawekezaji kutokana na kuwapo kwa taasisi zote muhimu Kituoni na kwamba
marekebisho yaliyotajwa na Waziri yatafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.
“Tumeyapokea maagizo ya Waziri na
tutayafanyia kazi, ni maagizo yenye tija kwa kituo” alisema Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Huduma za Mahala Pamaoja wa TIC Anna Lyimo.
Huduma za mahala pamoja kwenye
kituo cha uwekezaji Tanzania TIC zinajumuisha taasisi za Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Baraza la Taifa la usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC),
Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Shirika la viwango Tanzania
(TBS), Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Wizara ya Ardhi,
Idara ya Uhamiaji, Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA), Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA),
No comments:
Post a Comment