Meneja Masoko wa Kampuni ya SBC, Roselyne Kwelukilwa, akizungumza wakati
wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambako Wanawake wa jijini
Dar es Salaam waliiadhamisha kwenye Gym ya Body Fuel, Masaki.
(Picha na Tullo Chambo).
Baadhi ya Wanawake wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika Gym ya Body Fuel, Masaki.
NA MWANDISHI WETU
Baadhi ya Wanawake wakiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani katika Gym ya Body Fuel, Masaki.
NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuadhimisha siku ya Wanawake
Duniani, Klabu ya Mazoezi Body Gym Fuel kwa kushirikiana na kampuni ya SBC
Watengenezaji wa vinywaji baridi, wametoa fursa kwa wanawake kushiriki mazoezi
mbalimbali ya kujenga mwili na kuwaongezea kujiamini.
Akizungumza wakati wa programu hiyo, Meneja Masoko na Mauzo wa Body Gym Fuel Masaki jijini Dar es Salaam,
Chintal Kanabar, alisema kwa kutambua umuhimu wa wanawake katika jamii
imewasukuma kutoa fursa hiyo bure kwao.
Kanabar, alisema wanawake wameweza
kupata semina mbalimbali za kuwajengea uwezo, kushiriki mazoezi ya kujenga na
kuimarisha mwili bure wakiamini kuwa mwanamke ni mtu muhimu katika ustawi wa
jamii.
Naye Meneja Masoko wa SBC watengenezaji
wa vinywaji baridi vya Pepsi, Mirinda, Seven Up, Mountain Dew na hivi sasa maji
ya H2o, Roselyne Kwelukilwa, alisema kwa kuwa wanatambua umuhimu wa mazoezi kwa
jamii, ndicho kilichowasukuma kudhamini programu hiyo.
“Kama unavyoelewa mazoezi yana
faida nyingi kwa mwili wa binadamu na hususan sisi wanawake tunahitaji kuwa
fiti, wengine kupunguza uzito na kuweka miili sawa…Hivyo sisi kama mnavyoelewa
tuna kinywaji chetu cha H2o haya ni maji yenye ladha tamu hivyo tumeamua
kuwasapoti wanawake ili wazidi kujiweka fiti,” alisema.
Siku ya Wanawake Dunia huadhimishwa
kila Machi 8 Duniani kote na Body Gym Fuel kwa kushirikiana na SBC waliamua
kuidhimisha jana kwa programu hiyo.
No comments:
Post a Comment