HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 29, 2019

Prof. Ngowi aifagilia Serikali

 Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akichangia mada katika semina hiyo.
 Mhadhiri Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Emmanuel Akili, akichangia mada.
 Mkufunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Maige Mwasimba, akitoa mada katika semina ya Maendeleo ya Uchumi katika Sekta ya Usafiri na Usafirishaji.
 Dionizi Sabi, mmoja wa washiriki wa semina ya Maendeleo ya Uchumi katika Sekta ya Usafiri na Usafirishaji akichangia mada.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akichangia mada.
Mratibu wa semina semina Dk. Omary Swaleh (kushoto).

 Mmoja wa washiriki akipokea cheti.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akimkabidhi cheti, Dionizi Sabi, mmoja wa washiriki wa semina ya Maendeleo ya Uchumi katika Sekta ya Usafiri na Usafirishaji jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwakilishi wa Taasisi ya Kuehne Tanzania, Beatrice Milu.
 Picha ya pamoja.

NA JOHN MARWA

UONGOZI wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, umetoa pongezi kubwa kwa Serikali ya awamu ya tano kwa jitihada zake za kuboresha sekta ya usafiri na usafirishaji nchini.

Pongezi hizo zilibainishwa na Mkuu wa Chuo hicho Prof; Honest Ngowi wakati akizungumza na Tanzania Daima, baaada ya kufunga semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wataalamu wa taasisi mbalimbali.

Katika Semina hiyo iliyobeba maudhui ya Maendeleo ya Uchumi katika sekta ya usafiri na usafirishaji mijini, ilifanyika jijini Dar es Salaam kampasi ya chou hicho.

Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na taasisi ya Kuehne kupitia kampuni yake ya KUEHNE ya nchini Uswisi , wamekuwa wakiendesha semina mbali za kuwajengea wataalamu uwezo wa kutatua changamoto za sekta mbalimbali hapa nchini.

Alisema waliamua kuendesha semina hiyo kwa kutambua kuwa sekta ya usafiri na usafirishaji ni sekta mtambuka hivyo kila mtanzania napaswa kufahamu nin jinsi gani napaswa kushiriki katika kuendeleza sekta hiyo.

“Imekuwa ni semina nzuri kwani hawa watu ni wataalamu na wananafasi kubwa kuwajengea watanzania wengine uwezo kupitia taasisi wanazotoka ili kuweza kufikia malengo kuifanya sekta hii kuwa kitovu cha uchumi nchini.

“Tumefanikiwa kwani kile tulichohitaji kukifikisha tunaamini kimefika kwa asilimia kubwa, lakini pia tumegundua kwamba changamoto kubwa katika sekta hii mahitaji ni makubwa zaidi kuliko huduma inayotolewa,..alisema  Ngowi na kuongeza kuwa.

“Lakini pia, serekali yetu imejitahaidi sana kukabiliana na zinazoikabli sekta hii kwa kuanzisha UDART wamau ya kwanza nay a pili ambayo iko kwenye mchakato, na wako tayali kwenye mradi wa ujenzi wa treni za mwendokasi, wanahitaji pongezi licha ya changamoto bado zipo,” alisema.

Ngowi aliwapongeza washiriki wote na kuwaomba kufanyia kazi yale waliyoyapata katika semina hiyo kupitia makampuni yao na taasisi zao ili kukuza uchumi wa nchi.

Pia aliwaomba watanzania kuilinda miladi ya sekta ya usafiri  inayotengenezwa na seriakali na kuitumia vema katika kujijengea uchumi imara na kuweza kucahangia pato la taifa kwa kulipa kodi.

Aidha kwa upande wa taasisi ya Kuehne kupitia kwa mwakilishi wao hapa nchini Beatrice Millu alisema wanajisikia faraja kwa kuwa sehemu ya kuwajengea uwezo wataalamu mbali mbali katika kukabliana na changamoto za sekta hiyo hapa nchini.

“Sisi kama taasisi ya Kuehne kazi yetu kubwa ni kuwajengea watu katika mipango mikakati mabadiliko katika ukuwaji wa uchumi, nahapa nchini tunashirikiana na vyuo viwili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mzumbe.

“Tumefikia malengo kwani sasa ni miaka minne tunafanya nao kazi na kwa semina ambazo tumezito hadi sasa tumeona mabadiliko makubwa kwa watu kuibua changamoto ambazo tumekuwa tukiwafundisha,” alisema na kuongeza:

“Licha ya mafanikio tuliyoyafikia tumelenga kwenda mbali zaidi  kwa kuwafikia watanzania wengi zaidi hata wale wa hali ya chini, kama mama ntilie na wajasiriamali ili waweze kufahamu jinsi gani wanaweza kukabiliana na changamoto za sekta hii.

Taasisi ya Kuehne imekuwepo hapa nchini kwa miaka minne sasa lakini pia katika bara la afrika inashirikiana nan chi za Kenya, Rwanda, Nigeria, Seaneger na Seala Leon na Tanzania kupitia Chuo Kikuu Mzumbe  na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages