Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo
wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na Michezo, Yusuph Singo,
akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma kuhusu
kuliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu ya
Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ufanyike ndani ya siku 30 kuanzia
leo. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Bw.Alex Nkenyenge.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la
Taifa, Alex Nkenyenge, akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi
30, 2019 jijini Dodoma kuhusu kutekeleza maagizo ya Serikali kwa Baraza hilo kusimamia Uchaguzi ndani ya Klabu
ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ndani ya siku 30 kuanzia leo. Kushoto ni
Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari utamaduni Sanaa na
Michezo, Yusuph Singo.
Na Shamimu
nyaki –WHUSM
Serikali
imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kushirikiana na Shirikisho la mpira
wa Miguu (TFF) kuhakikisha uchaguzi ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans (Yanga) unafanyika ndani ya siku 30
kuanzia leo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Yusuph Singo katika
mkutano na Waandishi wa Habari leo Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa migogoro
iliyokuwepo huko nyuma imeshafika tamati hivyo uchaguzi ndani ya Klabu hiyo ni
lazima ufanyike.
“Nailekeza
BMT iwaelekeze TFF kuhakikisha taratibu zote za uchaguzi zinafuatwa na uchaguzi
ndani ya Klabu ya Dar es Salaam Young Africans unafayika ndani ya siku 30
kuanzia sasa”. alisema Bw. Singo.
Aidha
Bw.Singo amewahisi Viongozi, wanachama na wapenzi wa Klabu ya Dar es Salaam
Young Africans kutoanzisha migogoro wala vikwazo vingine bali kutumia siku 30
hizo kufanya uchaguzi ili kupata viongozi watakaoisimamia na kuiongoza Klabu
hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mpira wa miguu ndani na nje ya nchi.
Kwa upande
wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw.Alex Nkenyenge
amesema amepokea maagizo na atayafanyia kazi mara moja ili kipindi kilichowekwa
na Serikali cha siku 30 Klabu ya Yanga iwe tayari ina uongozi.
Bw.Nkenyenge
ameongeza kuwa atahakikisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF inapanga utaratibu
unaotakiwa kufuatwa kulingana na Katiba ya Shirikisho hilo ili Uchaguzi huo
ufanyike hatimaye migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya Klabu hiyo ifikie
mwisho na Klabu iendelee kufanya vizuri katika mpira wa miguu.
Klabu ya
Dar es Salaam Young Africans (Yanga) ni miongoni mwa Klabu kubwa za mpira wa
miguu hapa nchini ambayo kwa muda mrefu haijatekekeleza uchaguzi kwa mujibu wa
Katiba yao.
No comments:
Post a Comment