WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka Mawaziri wa Kilimo, Uwekezaji, Viwandana
Biashara, Mifugo na Uvuvi na Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto wakutane na wafanye mapitio ya taasisi zao na kuangalia maeneo
yanayogongana kiutendaji ili kila mmoja abaki na jukumu lake.
Ametoa
agizo hilo leo (Jumatano, Machi 6, 2019) alipotembelea Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kukagua
shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hizo na amewaagiza mawaziri
wakutane na wampelekee taarifa ya mapendekezo yao ifikapo Machi 30,
2019.
Hatua
hiyo imefikiwa baada ya kuwepo kwa malalamiko na manung’uniko kutoka
kwa baadhi ya wafanyabiashara ambao wamedai kuwepo kwa muingiliano wa
majukumu ya kiutendaji ya taasisi hizo, hivyo kuwasababisha washindwe
kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Waziri
Mkuu amesema taasisi hizo zinashughuli ambazo zinaingiliana na
kusababisha malalamiko kwa wateja wao, ambapo ametolea mfano suala la
kudhibiti ubora wa bidhaa ambalo linafanywa na TFDA na TBS kwa mujibu wa
sheria. Amewataka wapitie sheria zao na wajue ukomo majukumu yao.
“Kutaneni
pitieni maelekezo ya Serikali yanayoelekeza namna ya kuzifanya taasisi
hizi na zingine zinazofanya shughuli zinazofanana zilizo katika wizara
zenu bila kusanau Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (blue
print). Ifikapo tarehe 30 mwezi huu niwe nimepata mapendekezo yenu,”
amesisitiza.
Kadhalika,
Waziri Mkuu amewataka watendaji wa taasisi hizo wabadilike na waache
urasimu kwasababu hauna tija katika utekelezaji wa majukumu yao na
badala yake unaweza kuwayumbisha kwenye ufanyaji wao wa kazi. “Kila
mmoja atekeleze majukumu yake kwa uzingatia maadili ya taaluma yake.”
Pia,
Waziri Mkuu amewataka waangalie namna ya kuwahisha majibu ya vipimo vya
bidhaa wanazoletewa na wateja, kama watakuwa wamekamilisha kabla ya
siku za kisheria wawajulishe wateja wao na kuhusu sampuli ambazo
zitakuwa hazijaharibika wakati wa vipimo wawarudishie.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuzitaka taasisi hizo ziangalie namna ya
kusogeza huduma kwa wananchi kwa kuwa na watumishi katika ngazi za
wilaya na kwa TFDA ameitaka ianzishe maabara nyingine mbili kwenye kanda
ya Nyanda za Juu Kusini na ya Kaskazini ili kusogeza huduma kwa
wananchi.
No comments:
Post a Comment