NA TIGANYA VINCENT
WADAU wametakiwa
kuhakikisha wanaunganisha nguvu ili kuhakikisha kiwango cha maambukizi ya
malaria Mkoani Tabora kinashuka kutoka asilimia 11 katika eneo hilo na kufikia
kile cha Kitaifa cha asilimia 7.
Kauli hiyo imetolewa
leo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati akizundua Jukwa la
Mawasiliano ya afya kwa watu wazima(NAWEZA) kwa Mikoa ya Tabora , Arusha na
Singida.
Alisema hatua hiyo
itafanikiwa ikiwa kutakuwepo na mawasiliano baina ya wanajamii ili kutoa elimu sahihi itakayoasaidia
kubadili tabia kwa ajili ya kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa
Mwanri alisema jitihada
hizo zitasaidia kuwafanya watu wapate elimu juu ya kuangamiza mazalia ya umbu
na matumizi sahihi ya vyandarua kwa ajili ya kujikinga na umbu waenezao malaria
ili kuchangia malengo ya kitaifa ifikapo mwaka 2020.
Alisema kukosekana kwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya afya
kumewafanya wananchi mkoani hapa kutumia vyandarua kufugia kuku huku wengine
wakivitumia kutunzia bustani za mboga kwa kukosa elimu hivyo kushindwa
kubadilika.
Mwanri alisema wanajamii
ni vema wakaelimishwa juu ya kusafisha maeneo yao na kufukia madimbwi ya maji yanayozunguka
nyumba zao kama hatua ya msingi ya kukabiuliana na ugonjwa wa malaria badala ya
kusubiri waugue ndio elimu itolewe
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewavitaka vyombo vya habari kuisaidiana na Serikali
kufikisha ujumbe sahihi kwa wananchi ili wapate uelewa juu ya umuhimu wa
kuwa na afya bora itakayo wawezesha kushiriki kuinua uchumi wao na taifa
kwa ujumla.
Alisema kukosekana kwa taarifa sahihi zinazohusu masuala ya afya
kumewafanya wananchi wengi kukosa elimu hiyo hivyo kushindwa kubadilika.
Kufuatia hali hiyo Mwanri alisema kuwa vyombo vya habari
vinaowajibu mkubwa wa kuhakikisha vinafikisha elimu ya afya kwa wananchi.
Mwanri alisema kwamba wananchi wakipata taarifa sahihi kuhusu afya zao
watakuwa salama na vyombo vya habari ndivyo vinaweza kufikisha kwa haraka
ujumbe huo unaohusu afya zao.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa jukwaa la Naweza ni muhimu kwani linaleta
uhai mpya katika akili za wananchi ili waweze kuelimika na kubadilika.
Mwanri jitihada hizo
zitawezekana kama kutakuwepo na mawasiliano
ambayo yatawezesha kubadili tabia ili wananchi waweze kutumia huduma za afya
sahihi na kuwa tabia chanya kwa ajili ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.
Naye Mwakilishi kutoka
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto Oscar Kapera alisema Jukwaa la NAWEZA
linalenga kufikisha ujumbe unawajengea uwezo wananchi ili waweze kubadili tabia
zao za kiafya katika maeneo ya maambukizi ya VVU na mapambano dhidi ya Malaria.
Alisema maeneo mengine
ni pamoja na afya ya uzazi kwa lengo la
kumwezesha mama kujifungua salama na mtoto wake kuwa salama na mapambano dhidi
ya kifua kikuu.
No comments:
Post a Comment