Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazin
MAMLAKA ya Maji safi na Mazingira Arusha (AUWSA) imewatoa
hofu wakazi wa jiji la Arusha na maeneo inayotoa huduma juu ya uvumi wa taarifa
ya kuchafuliwa kwa maji ama kuchanganywa na
Majitakana kwamba taarifa hizo si za kweli .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano na Umma
wa Mamlaka ya Mazingira na Majitaka Arusha ,William Shayo ameeleza kuwa tayari
hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina juu
ya taarifa hiyo.
“Auwsa imechukua hatua za kufanya uchunguzi wa kina
ikiwahusisha wataalamu wa Maabara ya Maji mkoani Arusha,Sampuli za maji zilichukuliwa kutoka katika maeneo
mbalimbali yaliyo ripotiwa kwa
kuzingatia muongozo wa uchukuaji sampuli za maji”alisema Shayo.
Alisema Sampuli hizo zilipimwa katika maabara ya mkoa ya Wizra
ya maji na matokeo ya uchunguzi wa sampuli hizo umeonyesha kuwa huduma ya maji inayotolewa na Mamlaka hiyo ni
safi na yana dawa ya kutosha.
Mkurugenzi Mtendaji wa AUWSA , Luth Koye. |
“Kwa tahadhari Auwsa vile vile tumeamua kufanya Flushing
(kusafisha) ya mfumo mzima wa
majisafi kwa sehemu maalumu zilizopo kwenye mtandao ,ambazo
zilisanifiwa kwa ajili ya kazi hiyo.”alisema Shayo.
Shayo alisema Auwsa pia imeendelea kuchukua sampuli katika
maeneo mengine kwa kadri wanavyopokea taarifa na kwamba vipimo vya sampuli hizo vimeonesha maji hayo ni safi
na yana dawa ya kutosha.
Mbali na uchukuaji wa Sampuli na ufanyaji wa vipimo ,Shayo
alisema Auwsa imetembelea maeneo mbalimbali ambayo kumekuwa na taarifa za uwepo
wa maji hayo na kutoa elimu juu ya uhifadhi salama wa maji kwa matumizi salama.
Aidha Shayo alisema kwa yoyote mwenye taarifa zaidi kuhusu
uvumi ulioenezwa kwenye mitandaoo ya kijamii awasiliane na Mamlaka ya Majisafi
na Mazingira Arusha (AUWSA) kupitia namba 0800110069 ambazo ni bure au 0755900693.
No comments:
Post a Comment