Askari wa Usalama Barabarani akiongozi vikundi mbalimbali vya wanawake wa Manispaa ya Tabora kuingia katika Uwanja wa Chipukizi ili kushirikia Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duaniani. (Picha na Tiganya Vincent).
NA TIGANYA VINCENT
NA TIGANYA VINCENT
WANAWAKE ambao wamenufaika na mikopo ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora wametakiwa kuhakikisha wanarejesha mikopo wanapewa kwa wakati ili fedha hizo ziweze kuvinufaisha vikundi vingi katika kujiletea maendelea kama ilivyokusudiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Janat Kayanda katika katika Uwanja wa Chipukizi Manispaa ya Tabora ikiwa maadhimisho ya siku ya wanawake.
Alisema fedha zinazotolewa na Halmashauri sio sadaka na wala sio ruzuku ya Serikali kwao ,bali zinatakiwa kurejesha ili ziweze kukopeshwa kwa wengine.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri aliuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kuanza utekelezaji wa maagizo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kiwango cha mikopo kiwe kikubwa ambacho kitaleta tija kwa vikundi.
Alisema kufuatia agizo kiwango cha mikopo kwa vikundi ni lazima kianzie milioni 15 ili wahusika waweze kuzalisha bidhaa bora badala ya kutoa fedha kidogo ambazo zinaiishia kwa wanakundi kugawana.
Mwanri alisema hatakubaki kuona kikundi kinapata mkopo wa shilingi milioni 1.5 kwa kuwa fedha hizo haziwezi kuwasaidia wanakikundi kupata maendeleo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kuhakikisha wanawatafutia eneo rafiki ambalo Wajasirimali watafanya shughuli zao.
Katika hatua nyingine Katibu huyo wa CCM Mkoa wa Tabora aliendesha harambee kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo ambapo kiasi cha milioni 3.5 zilipatikana kwa ajili ya kuwasaidia wajasirimali wanawake wa Manispaa ya Tabora.
No comments:
Post a Comment