MTENDAJI
Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPBL) Boniface Wambura (pichani), amejibu
mapigo kwa malalamiko ya ratiba ya Lgi hiyo akibainisha kuwa kila timu
itacheza mechi 38 hivyo hakuna klabu inayopendelewa.
Wambura
ameyasema hayo ikiwa ni siku moja tu mara baada ya Kocha Mkuu wa Yanga
SC kutoa malalamiko ya kubanwa na ratiba ya Ligi huku watani wao SC
wakiwa na viporo zaidi ya 10 wakati ambao baadhi ya klabu zimebakiza
mechi nne kumaliza Ligi.
Zahera
alisema wachezaji wake wanachoka sana licha ya kutumia usafiri wa Ndege
kwa sababu michezo iko karibu karibu na haiwapi nafasi ya kupumzika.
Pia
zahera alionyeshwa kushangazwa na michezo waliyobaki nayo wapinzani wao
Simba SC kwa kuwa na michezo zaidi ya 10 ambayo hawajacheza hali
inayompa ukakasi na kusisitiza kuwa ligi iko mwishoni wanapaswa Wekundu
hao kucheza mechi hizo waweze kuwa sawa.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Wambura alisema nikweli msimu huu
wamekabiliwa na changamoto ya ratiba jambo ambalo limekuwa nje ya uwezo
wao kwa uwepo wa mashindano mengi kwa baadhi ya klabu.
“Changamoto
za ratiba ni kweli zipo, na tunazitambua, lakini lazima tukubali kuwa
mabadiliko ya ratiba ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho ndo yameiasili
zaidi ratiba yetu.
“Michuano
hiyo ya CAF imekuwa ikifanyika kuanzia mwezi Novemba lakini sasa, CAF
waliamua kubadilika na kuja kwenye mfumo wetu wa kuanza Mwezi August na
kumalizika mwezi May,”amesema na kuongeza kuwa.
“Licha
ya mabadiliko hayo ya CAF lakini tunmekuwa na kombe la Sport Pesa na
kombe la Mapinduzi nayo yaliingia hapa kati, imekuwa ni changamoto kwetu
pia ongezeko la timu kutoka 16 hadi 20 nayo imekuwa ni changamoto ukiwa
ni msimu wetu wa kwanza kuwa na timu 20.
“Pia
kama Taifa tulijipanga kwa timu yetu ya Taifa Taifa Stars kufuzu
fainali za AFCON jambo ambalo tumefanikiwa na hili lilikula muda wa ligi
kwani kuna wakati tulitumia hadi siku 21 kwa ajili ya maandalizi ya
Timu hiyo.
“Pamoja
na changamoto hizo limekuwa ni somo kwetu na tunaahidi kuwa msimu ujao
tutakuja na ratiba ambayo haitakuwa na ukakasi kwa kila mmoja, na
malalamiko yanayotolewa jamani kila timu itacheza mechi 38 hakuna
itakayo cheza michezo 30,”amesema.
Lakini
pia Wambura aliongeza kuwa kesho watatoa ratiba ambayo itaonyesha ni
jinsi gani Simba watacheza viporo vyao na Ligi iwezealizika kwa wakati.
“Tumekaa
vikao na kupitia ratiba na kesho tutatangaza ratiba ambayo itaonyesha
jinsi gani Simba na klabu nyingine zitakavyo cheza viporo vyao, ni wazi
kuwa Simba watakuwa na ratiba ngumu sana na watapitia wakati mgumu
lakini yote lazima tuhakikishe Ligi inamalizika mwezi May,”amesema.
Wakati
wambura akitoa utetezi huo Mabingwa watetezi wameshuka dimbani mara 22
huku vinara wa ligi hiyo wakicheza mechi 30 hadi sasa.
Tayari kuna klabu zimeshacheza michezo 33 zikisaliwa na mechi tano kumaliza ligi huku Simba wakisaliwa na michezo 16 mkononi.
Simba
wanakabiliwa na kibarua kizito jumamosi hii robo fainali ya pili ya
Ligi ya Mabingwa Afrika CAF CL dhidi ya TP Mazembe mjini Lubumbashi
wakihitaji ushindi ama sare ya mabao kutinga nusu fainali.
Swali
ni je kama Simba wanafanikiwa kutinga nusu fainali TPBL watakuja na
ratiba gani kuhakikisha viporo vya Simba vinachezwa na ligi inamalizika
kwa wakati.
No comments:
Post a Comment