Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Umma wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam Dr. Arnold Towo akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari
Mt. John Paul II ya Kahama Mkoani Shinyanga walipofanya ziara ya masomo kwa
vitendo katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam tarehe 12 Aprili, 2019.
Bi Elizabeth Chuwa kutoka Kurugenzi ya Masomo ya
Shahada ya Awali akiwaeleza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul
taratibu za kujiunga na chuo Kikuu cha Dar es salaam wakati wa ziara fupi
iliyofanywa na shule hiyo ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo katika
Kitengo cha Huduma kwa Umma cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mt. John Paul II ya
Kahama Mkoani Shinyanga wakisikiliza kwa makini kuhusu huduma zinazotolewa na
Chuo kikuu cha Dar es Salaam wakati wa ziara waliyofanya katika Kitengo cha
Huduma kwa Umma.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaelekeza wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Mt. John Paul ya Kahama namna kabati la Kielektroniki linavyotumiwa na
wanafunzi wanapoingia Maktaba wakati wa kujisomea.
Msaidizi wa Maktaba Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Dickens Dominic akiwafafanulia jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya John
Paul II wakati wa ziara ya kimasomo waliyofanya kujionea namna Maktaba mpya
inavyofanyakazi.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Maktaba Mpya ya Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam Ernest Nyari akiwaonesha wanafunzi (Hawapo pichani) moja ya
Vitabu vya Sayansi vinavyopatikana katika chumba cha Maktaba mahususi kwa ajili
ya masomo ya Sayansi kiitwacho " Science Collection" wakati wa ziara
fupi iliyofanywa na shule ya Sekindari ya Mt. John Paul II katika Chuo Kikuu
Cha Dar es salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma (
Mwenye shati la Bluu) pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Kitengo cha Huduma kwa Umma na Maktaba Mpya wakiwa katika Picha ya Pamoja na
Wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Mt. John Paul II kutoka Kahama
Shinyanga baada ya ziara fupi katika Maktaba hiyo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Umma Dk.
Arnold Towo amewaeleza wanafunzi wa Kidato cha I hadi 6 wa Shule ya Sekondari
ya Mt. John Paul II kutoka Kahama Mkoani Shinyanga kuzingatia vema masomo yao ili kuwa na msingi bora wa
elimu na kuweza kuchagua masomo yao vema ili kukidhi mahitaji yao wanapofikia
hatua ya kujiunga katika Masomo ya Shahada za juu.
Amesema hayo wakati wa ziara fupi iliyofanywa na
uongozi wa shule ya Mt. John Paul II pamoja na wanafunzi 55 walipotembelea Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo na kufahamu
utendaji kazi wa Chuo Kikuu Mlimani.
"Napenda kuwasisitiza wanafunzi kutumia muda wao
vema wa masoma, kujituma na kujifunza vitu tofauti pamja na kutambua mapema
kile unachotaka kusomea ili inapofika wakati wa kujiunga na chuo kikuu wawe wamejitambua
na kufahamu vema wanataka kusoma nini, alisisitiza Dr. Towo.
Miongoni mwa vitu walivyojifunza wakati wa ziara ni
pamoja na kufahamu taratibu na vigezo vya kujiunga na Chuo kikuu cha Dar es
Salaam kutoka kurugenzi ya masomo ya Shahada ya awali, masuala ya uhandisi wa
umeme na kupata kupata ufafanuzi kuhusu masuala ya historia ya Afrika pamoja na
kutembelea na kuona jinsi maktaba mpya inavyofanyakazi.
Dr. Towo aliongeza kuwa, kikubwa katika masomo
wanafunzi wanatakiwa kuwa na ujuzi wa juu na ufaulu bora na wenye uwezo wa
kujieleze ili kukidhi hitaji la soko pale wanapohitimu masomo yao ya juu.
"Lengo kuu la ziara hii kwa wanafunzi wetu ni
kuwajengea uwezo na kuona kwa vitendo yale wanayosikia kuhusu chuo kikuu cha
Dar es Salaam pamoja ikiwa ni sehemu ya kuwapa hamasa ya kujituma katika masomo
pale wanaporejea shuleni", alisema Mwalimu
Enock Julius.
Chuo Kikuu Cha Dar es salaam kinatoa huduma kuu tatu
ambazo ni Kutoa Elimu, Kufanya Tafiti pamoja kutoa huduma za ushauri kwa
Mashirika ya umma pamoja na Sekta binafsi.
Imetolewa na Afisa Uhusiano
Kitengo cha Huduma kwa Umma
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Tarehe 13 Aprili,2019
No comments:
Post a Comment