Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo Omar Singo (aliyevaa koti) akimkabidhi mchezaji
wa zamani wa Taifa Stars Amri Kiemba mpira wakati wa hafla ya uzinduzi
wa kampeni maalum ya DStv Inogile ambayo pia inalenga kuhamasisha umma
kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17 yanayoanza mwisho wa wiki hii.
Wengine wachezaji wa zamani wa Taifa Stars na maafisa waandamizi wa
MultiChoice Tanzania. Miongoni mwao ni Dua Said,
Lubigisa Madata, Edibily Lunyamila, Amri Kiemba, Mohammed Hussein na
Fikiri Magoso na Sekilojo Chambua.
Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo Omar Singo (aliyevaa koti) akiwa katika picha
ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars) na
maafisa waandamizi wa MultiChoice Tanzania wakati wa hafla ya uzinduzi
wa kampeni maalum ya DStv Inogile ambayo pia inalenga kuhamasisha umma
kwa ajili ya mashindano ya AFCON U17 yanayoanza mwisho wa wiki hii.
kutoka kushoto (waliasimama) ni Dua Said, Lubigisa
Madata, Edibily Lunyamila, Amri Kiemba, Mohammed Hussein na Fikiri
Magoso. Kwa waliokaa ni Sekilojo Chambua, Ronald Shelukindo na Salum
Salum.
Dar es Salaam, Tanzania
Katika kuhakikisha kuwa Tanzania
inaendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya kimataifa na Watanzania
kushuhudia mubashara timu yao DStv imetangaza rasmi kuwa itarusha
mubashara michuano ya kombe la AFCON U17 2019 na hivyo kutangaza kampeni
maalum ya kuhamasisha ushindi kwa timu yetu ya
Serengeti Boys!
Akizungumza
katika hafla ya kuzindua kampeni hiyo ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv
Inogile’, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Ronald Baraka
Shelukindo
amesema kuwa katika kuunga mkono kampeni ya kuifanya nchi yetu ifanye
vizuri katika michezo mbalimbali, DStv imehakikisha kuwa michuano
mbalimbali ya kimataifa inarushwa mubashara tena katika kifurushi cha
chini kabisa cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu - hivyo
kuwawezesha mamilioni ya watanzania kuziona timu zetu na hivyo kuongeza
ari ya kuziunga mkono kwa hali na mali.
Kwa
upande wa michuano ya AFCON ya vijana inayoana mwishoni mwa wiki hii,
Shelukindo amesema DStv itakuwa ikifanya kampeni kwa njia mbalimbali
ikiwemo
kwa njia ya mitandao na matangazo mbalimbali kuhamasisha na kuitia
nguvu timu ya taifa ili iweze kufanya vizuri
“Hili
ni swala la kitaifa, hivyo tunataka watanzania popote walipo waweze
kushuhudia timu yetu ikipambana kwa ajili ya sifa ya nchi yetu” alisema
Shelukindo
na kuongeza kuwa DStv inaonekana kote barani Afrika hivyo kitendo cha
kuonyesha michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya kwanza hapa nchini
kitaufanya ulimwengu kuyashuhudia mashindano hayo na pia kuitangaza
nchi yetu. “Kwa michuano hii kuonekana DStv,
ina maana kubwa sana kwa nchi yetu, hii ni njia moja wapo pia ya
kuitangaza nchi yetu na Afrika na dunia nzima itambue kuwa na sisi tuna
uwezo siyo tu wa kuandaa mashindano haya bali pia wa kuyaonyesha”
Naye
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Dr. Omar Singo amesema kuwa kitendo
cha DStv kuonyesha mubashara michuano hiyo ni cha kupongezwa kwani ni
sifa
kubwa kwa nchi yetu. Pia amesema mchango mkubwa unaotolewa na
MultiChoice Tanzania katika sekta ya michezo umechangia sana katika
kukuza michezo na kuliletea taifa sifa kubwa.
“Serikali
inathamini sana michango ya aina mbalimbali inayotolewa na wadau kama
DStv katika kukuza michezo hapa nchini. Tunaamini kuwa kwa ushirikiano
huu mafanikia haya ambayo tumeanza kuyapata yataendelea na tutafikia
azma yetu ya kuwa taifa kubwa kimichezo duniani” alisema Dr. Singo
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wenzake waliowahi kuichezea timu ya Taifa –
Taifa Stars ambao walishiriki katika hafla hiyo, mchezaji machachari
Amri Kiemba moja kati ya wachezaji nguli waliowahi kuichezea timu ya
Taifa ya Tanzania kwa miaka ya nyuma aieleza kuwa , “Kwa mara ya kwanza
Tanzania imepewa heshima kubwa kuyaandaa mashindano haya makubwa hivyo
ni wajibu wetu sisi watanzania kuonyesha uzalendo
na kuwatia moyo vijana wetu ili kuhakikisha wanashinda katika michuano
hii na kupata tiketi ya kwenda kwenye mashindano ya dunia nchini
Brazil”. Wanasoka wengine nguli walioshiriki katika hafla hiyo ni Fikiri
Magoso, Dua Said, Lubigisa Madata, Amri Kiemba,
Edibily Lunyamila na Sekilojo Chambua
Mbali
ya michuano ya kombe hili la vijana wa chini ya miaka 17 itakayoanza
hivi karibuni, wateja wa DStv pia wataendelea kufurahia maudhui
mbalimbali
zikiwemo sinema na tamthilia mbalimbali kutoka nje na hapa nyumbani
kama vile msimu mpya wa vichekesho vya Kitimtim, tamthilia ya HUBA,
Rebeca kipindi maarufu cha Shilawadu Xtra na bila kusahau kipindi kipya
cha Maisha Yangu kinachoelezea maisha na mapito
ya watu mashuhuri kutoka hapa nyumbani Tanzania vyote vikiwa
vinapatikana kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo iliyopo katika
kifurushi cha Bomba.
No comments:
Post a Comment