HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 11, 2019

HALOTEL YAZINDUA HUDUMA MPYA YA TOMATO PLUS

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya TOMATO PLUS jijini Dar es Salaam leo.

NA CONSTANCIA NKINDI

KAMPUNI ya Mawasiliano ya simu ya Halotel, imeendelea kuongeza thamani na ubunifu katika mawasiliano kwa kuzindua huduma mpya iliyoboreshwa ili kuwawezesha wateja wake nchi nzima kufurahia mawasiliano ya mtandao wa Halotel pekee.

Huduma hiyo mpya inayojulikana kwa jina Ia TOMATO PLUS itamuwezesha mteja wa Halotel kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga pale atakapojiunga na huduma ya Tomato Plus.

Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda, amesema huduma hii ni ya wateja wote wa Halotel na Mteja akijiunga na huduma ya Tomato Plus, anaweza kuongea kwa dakika tano za mwanzo bure mitandao yote kwa kila simu atakayopiga.

“Huduma hii imeboreshwa zaidi kwa kuzingatia mahitaji ya wateja wetu katika mawasiliano ili kuwawezesha kuwasiliana bila kikomo kwa kupiga simu mitandao yote na kuongea kwa dakika 5 za mwanzo bure kwa kila simu watakayopiga” alisema Semwenda.

“Mteja wa Halotel anaweza kujiunga na kufurahia huduma hii kwa kupitia menu yetu ya kwaida ya *148*66# na kasha atachagua namba namba 8 ambapo ataweza kujiunga kwa siku, wiki au mwezi na kufuraha huduma ya Tomao Plus wakati wowote na mahali popote.” Alisema na kuongeza Semwenda.

Huduma ya TOMATO PLUS imelenga katika kuongeza ufanisi, nafasi na uwezo wa mawasiliano kwa wateja wa Halotel na kwa watanzania wote, wakiwemo wafanya biashara, wafanyakazi wa sekta binafsi na serikali na wateja wengine walioko sekta zingine mijini na kuwasiliana na kupata taarifa mbali mbali kwa uhakika.

No comments:

Post a Comment

Pages