Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kupotea msaada wa Tablets na vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Mradi RARIS kwa kupitia UNDP na ESRF, leo Jijini Dodoma, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe na kwa upande wa kulia ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Natalie Boucly.
Mratibu wa Mradi wa RARIS kutoka ESRF Dkt.Osward
Mashindano akitoa taarifa ya namna Mradi
wa Kilimo wa RARIS utakavyorahisha upatikanaji wa taarifa muhimu za wakulima kwa Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga (hayupo pichani) katika hafla
ya kukabidhi vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa
kupitia mradi huo unaofadhili na UNDP pamoja na ESRF leo Jijini Dodoma.
Waziri wa Kilimo
Mhe.Japhet Hasunga (wa sita
kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Bodi mbalimbali ya
mazao ya Kilimo mara baada ya kupokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyokuwa
vikitolewa na UNDP/ESRF kupitia mradi wa RARIS uliyodhaminiwa na Shirika la
Maendeleo ya UNDP, ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP Natalie Boucly (wasaba kulia)
na Katibu Mkuu Wizara Kilimo Mhandisi
Mathew Mtigumwe (wasita kulia) leo jijini Dodoma.
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Serikali
imetoa agizo kwa Wakurugenzi wa Bodi za Mazao ya Kilimo nchini kukamilisha
Kanzi Data ya wakulima wote itakayowawezesha wakulima hao kutambulika kwa
urahisi.
Agizo
hilo limetolewa leo jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati
alipokuwa akipokea msaada wa vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Shirika la Maendeleo la Umoja
wa Mataifa (UNDP) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF)
kupitia mradi wa RARIS.
Hasunga
amesema kuwa muda umefika ambapo ni lazima nchi iwe na Kanzi Data ambayo
itaonyesha taarifa zote za wakulima zikiwemo za kutambua idadi ya wakulima,
eneo wanalofanyia kilimo,aina ya mazao yanayolimwa pamoja na kufahamu wakulima
wakubwa, wakati na wadogo pia itasaidia kuweka mipango endelevu na kufanya
maamuzi sahihi kwa wakulima hao.
"Imefikia
wakati wakulima nao watambulike na kupewa vitambulisho, tulishakaa vikao na
Bodi zote za mazao kujadili suala hilo hivyo natoa agizo kuwa ifikapo Juni 30
mwaka huu Bodi zote ziwe na Kanzi Data za wakulima isipokuwa Bodi ya Nafaka na
Mazao Mchanganyiko ambayo Kanzi Data
yake itachukua muda kidogo kukamilika kwa sababu ya kuwepo kwa mazao
mchanganyiko." alisema Hasunga.
Hasunga
ameongeza kuwa hadi kufikia muda huu, uandikishaji wa wakulima hao unaridhisha
kwani kufikia Machi, 31 mwaka huu,
uandikishaji huo umefikia takribani asilimia 72 ambapo jumla ya wakulima
1,274,337 kati ya lengo la makadirio ya wakulima 1,700,000 wamefikiwa.
Aidha,
Hasunga amefafanua kuwa ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na tija, lazima
kuhakikisha tunaanzisha Bima ya Mazao
ambayo itasaidia kilimo nchini kuwa na ulinzi hata ikitokea changamoto yoyote
kwa wakulima lazima walipwe fidia kama biashara zingine zinazofanyika.
Akielezea
kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Mratibu wa Mradi, Osward Mashindano amesema
kuwa mradi huo ulianza mnamo Oktoba, 2018 na unatekelezwa kila baada ya miezi
mitatu ambapo kwa sasa wanaandaa utekelezaji kwa mara ya tatu.
"Kupitia
mradi huu Shirika la UNDP na ESRF wametoa msaada wa vifaa kwa ajili kurahisisha
utendaji kazi wa wizara hiyo vikiwemo vya vishikwambi 50, Kompyuta mpakato tatu,
printa mbili pamoja na vifaa viwili vya kurekodia", alisema Mashindano.
Kilimo
ndio msingi wa maendeleo, takwimu zinaeleza wazi kuwa kilimo kinatoa mchango
mkubwa kwenye maendeleo ya nchi ambapo
kinachangia asilimia 28.1 ya Pato la Taifa, asilimia 30 ya fedha za kigeni.
asilimia 65.5 ya ajira zote zilizopo hapa nchini, asilimia 66 za malighafi
zinazohitajika viwandani pamoja na asilimia 100 ya chakula.
No comments:
Post a Comment