Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amefanya ziara ya
ukaguzi wa miradi mbalimbali wilaya ya Kigamboni ambapo amewaagiza
Wakala wa Majengo ya serikali TBA kuhakikisha wanakamilisha Mara moja
ujenzi wa majengo ya Halmashauri ya wilaya ya Kigamboni, Ofisi ya Mkuu
wa wilaya na Nyumba za viongozi kabla ya Juni 30 mwaka huu.
Makonda
amesema endapo wakala hao watashindwa kutekeleza agizo hilo
watachukuliwa hatua ikiwemo kunyang'anywa mradi, kurudisha fedha
iliyobaki na watalazimika kulipa kodi ya jengo la mtu binasi
linalotumiwa kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.
"Nimekuchukizwa
na hali ya kusuasua kwa mradi huo licha ya kuongezewa muda zaidi ya
mara mbili na fedha zote za ujenzi mlishapatiwa jambo linalopelekea
serikali tunatumia mamilioni ya pesa kulipa kodi ya pango kwenye jengo
la mtu binafsi linalotumika kama ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kigamboni,
na endapo mtashindwa kutekeleza
agizo hili nitachukua hatua ikiwemo kuwanyang'anya mradi,kurudisha fedha
iliyobaki na mtalazimika kulipa kodi ya jengo la mtu binasi
linalotumiwa kama Ofisi ya Mkuu wa Wilaya"anasema Makonda.
Akiwa
katika mradi wa ujenzi wa jengo la Hospital ya Wilaya ya Kigamboni
Makonda ameridhishwa na kasi ya ujenzi huo na kuagiza mkandarasi kufanya
kazi usiku na mchana kuhakikisha jengo linakabidhiwa kabla ya Juni 30
mwaka huu.
Kwa upande
wake Mratibu wa Wakala wa Majengo ya serikali Mkoa wa Dar es salaam
Mhandisi Wilson Tesha amemuahidi RC Makonda kuwa wakala hao
watakahikisha wanakamilisha ujenzi kabla ya Juni 30 kama walivyoagizwa.
No comments:
Post a Comment